Maiti
ya Kijana Rashid Juma aliyepigwa risasi na askari polisi ikiwa imelazwa katika
chumba cha kuifadhia katika hospitali ya Wilaya ya Bukombe.
BUKOMBE
Mtu mmoja anayeitwa
Rashid Juma (23) ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi katika kitongoji
cha Kilimahewa kilichoko mjini Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoani Geita leo(Nov
24) Asubuhi.
Marehemu Juma
amedaiwa kupigwa risasi na askari polisi wakati walipokuwa wanakamata mtu,
anayesadikiwa kuwa ni jambazi, aliyekuwa amejificha kwenye nyumba moja katika
kitongoji hicho.
Mwandishi wetu
ameripoti kuwa, baada ya askari kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, wananchi wenye
hasira walilivamia gari la polisi kwa nia ya kumuua, hali iliyosababisha askari
waanze kupiga risasi za juu ili kuwatawanya.
Imeelezwa kuwa
katika tafrani hiyo, marehemu aliokotwa na wananchi akiwa amejeruhiwa kiunoni
kwa kitu kinachohisiwa kuwa ni risasi ya moto, kabla ya kubebwa na wananchi hao
kwa maandamano hadi kituo cha polisi.
Mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo Dk. Archard Rwezahura ameleza, marehemu Juma amefariki kabla
yakufikishwa hospitalini hapo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Geita Lenard Paul amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba hatua
za kisheria zinafuatiliwa.
MATUKIO KATIKA
PICHA
Askari
polisi akijitahidi kuwatawanya wananchi waliokuwa na hasira
Moshi
wa bomu la machozi ambalo lililirushwa na askari polisi wa kituo hicho kwa ajili
ya kuwatawanya wananchi ambao walikuwa na lengo la kuvamia kituo.
Msafara
wa Mbunge, wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi Pamoja na Diwani na baadhi ya
askari na wananchi wakiwa wanaongozana kwenda katika hospitali ya Wilaya ya
Bukombe kwa ajili ya kuangalia mwili wa marehemu Rashid Juma aliyepigwa risasi
na polisi na kufa hapo
Mbunge wa Bukombe
Profesa, Kulikoyela Kahigi Chadema (Kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dk. Archard Rwezahura, (aliyevaa shati la
kitenge) jinsi alivyopokea maiti ya kijana huyo ambaye alipigwa risasi na Polisi
na kufikishwa hospitali hapo akiwa amefariki.
SOURCE SHOMARI
BINDA BLOG
Post a Comment