Haki za watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini kwa mujibu wa kanuni za usafirishaji za mwaka 2007 gn.218/2007
1. Haki ya kurudishiwa nauli chombo cha usafiri kinapochelewa kuanza safari saa mbili baada ya muda uliopangwa kwenye ratiba na tiketi (Kanuni No. 21-(2) ).
2. Haki ya kupewa tiketi ndani ya ofisi ya mtoa huduma ya usafiri husika na siyo vinginevyo (Kanuni ya 17-(1p) na ya 24-(1) ).
3. Haki ya kutonyanyaswa kwa lugha za matusi au vitendo vyovyote kinyume na taratibu au kwa mujibu wa haki za binadamu iwe kwa abiria mtu mzima au mwanafunzi (Kanuni ya 18-(1a,g,h) ).
4. Haki ya kufikishwa mwisho wa safari yaani kituo husika anakoelekea abiria (Kanuni ya 18-(1d) ).
5. Haki ya kutosimamishwa ndani ya chombo cha usafiri (kwa mabasi ya mikoani) awapo safarini (Kanuni 17-1f) ).
6. Haki ya kulipa nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka yaSUMATRAna si zaidi ya kiwango husika (Kanuniya 34-1,2,3) ).
7. Haki ya kutoendeshwa na dereva mmoja (kwa mabasi ya mikoani) zaidi ya saa nane (Kanuni ya 17-1g).
8. haki ya kulindwa kwa mikanda ya usalama (Passengers seat belt) wakati wote wa safari (Kanuni ya 17-1i).
9. Haki ya kupata huduma muhimu za usafi, afya na taarifa zinazohusiana na safari yake (Kanuni ya 17-1l,m,n).
10. Haki ya kutolipia mzigo usiozidi kilogramu ishirini kwa mtu mzima na kilogramu kumi kwa mtoto (Kanuni ya 23-1,2).
11. Haki ya kurudishiwa nauli yote abiria pale anapohailisha safari saa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa safari wa chombo husikakamailivyoainishwa kwenye tiketi na ratiba (Kanuni ya 24-1,2,3).
12. Haki ya kuhifadhiwa/kutunziwa vifaa au mali ya abiria vinapothibitishwa kusahaulika ndani ya chombo cha usafiri husika (Kanuni ya 38).
13. Haki ya kurudishiwa nauli pungufu ya asilimia kumi na tano tu ya kiasi alicholipakamailivyoainishwa kwenye tiketi endapo abiria atavunja safari ndani ya muda chini ya saa ishirini na nne kabla ya muda wa chombo cha usafiri kuanza safari (Kanuni ya 24-3).
Imeandaliwa na Johary Kachwamba kwa hisani ya mtandao wa Sumatra.
Post a Comment