Wimbo wa "Mama Kimwaga" wa
Ngoma Africa band
Wazua baraha ! Jimama Pesa
lamsaka Kamanda Ras Makunja wa FFU ! kwa bakora mitaani
!
Bremen,Ujerumani.
Katika hali ya utatanishi kiongozi
wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta akipewa
mashaka ya maisha na mwanamama moja kisa
wimbo "Mama Kimwaga" ! ambao takribani mwezi mzima wimbo huo na nyingine za
bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa mara na kituo cha Radio Funk haus inayorusha
matangazo mjini Bremen,Ujerumani.
Mwanamama huyo ambaye aliguswa
sana na ujumbe wa wimbo huo, aliamua kutinga katika ukumbi wa mazoezi wa bendi hiyo
mjini Oldenburg,mkononi akiwa na bakora ! mdomoni yakiwa yanamtoka
maneno ya
hasira.
Alisikika
Mama huyo akidai kuonana na mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa aka FFU kamanda
Ras Makunja,kwa bahati mbaya alijibiwa na wanamuziki waliokuwa eneo hilo, kuwa
Kamanda hayupo.
Baada ya kupata jibu hilo, Mama
huyo na kuulizwa kulikoni? Jimama Pesa huyo alisikika akidai kuwa
alikuja kumtia adabu Kamanda Ras makunja wa FFU.
Jimama pesa huyo aliendelea
kukoroma na kutema kibesi kuwa wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ujumbe wake unamnyima
raha jimama huyo mwenye kuongea kiswahili fasaha kinachoonyesha
kuwa anatoka nchi jirani kwa watani wa jadi wa Tanzania.
Aidha Jimama pesa huyo, amedai
kuwa akutegemea kabisa kama wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ungepelekwa tena kwa
maDJ wa redio Bremen na kurushwa hewani Ujerumani kote kwa kupitia sauti
ya Funk Haus Europa, wanamuziki aka "maafande" wa Ngoma Africa band wakimtetea
Boss yao Kamanda Ras Makunja,wamedai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa ma Dj wa
redio kwa CD hiyo ilikuwapo pale redio siku
nyingi,na katika CD hiyo aliyeimbwa ni "Mama Kimwaga" sasa inakuaje ? kamanda
asakwe na bakora ka kushutumiwa kuwa
anazuia ridhiki ya mahitaji ya starehe ya jimama pesa
huyo.
Wanamuziki wa
ngoma africa wanamuhoji mwanamama anayemsaka kwa bakora kamanda wao
Ras Makunja,ambaye mara nyingi anadaiwa kuwa ni mtunzi na mwimbaji mwenye
darubini kali. UNAWEZA KUUSIKILIZA WIMBA HUO
KUPITIA www.myspace.com/thengomaafrica na www.reverbnation.com/ngomaafricaband
Post a Comment