KLABU ya Yanga leo imemtangaza Shaaban Katwila kuwa
Meneja wa Timu A na Baraka Kizuguto kuwa Afisa Mawasiliano wa klabu, kujaza
nafasi zilizkokuwa wazi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mkuu wa
klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako, amesema kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichoketi mwishoni mwa wiki kiliwapendekeza Katwila na Kizuguto kushika nafasi
hizo zilizokua wazi.
Katwila anakuwa Meneja wa timu kufuatia kuwa wazi kwa
nafasi hiyo baada ya aliyekuwa meneja wa timu Hafidh Saleh kuhamishiwa idara ya
Mipango na Usafirishaji na Kizuguto anachukua nafasi iliyokua wazi kufuatia
Louis Sendeu kumalizika kwa mkataba wake.
Aidha Mwalusako alisema Katwila ana uzoefu na masuala
ya mpira, alikuwa mchezaji wa Yanga kwa kipindi kirefu, alikuwa Nahodha wa timu
ya Yanga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa vipindi tofauti hivyo anauelewa na
masuala ya mpira na atakua kiunganishi kizuri kati ya Uongozi na
wachezaji.
Kizuguto ana taaluma ya Teknlojia, Habari na
Mawasiliano hibyo Kamati ya Utendaji iliona anafaa kushika nafasi ya Habari na
Mawasilliano, kwa kuwa ana uzoefu na masuala ya mawasiliano ya jamii kufuatia
kazi hiyo kwa muda mrefu alisema 'Mwalusako'
Naye Katwila alishukuru kwa uongozi kumwamini na kumpa
nafasi hiyo, na kusema anaamini ataifanya vizuri ipasavyo kwa kuwa ana uzoefu na
masuala ya michezo na uongozi.
Afisa Mawasiliano mpya wa Yanga Kizuguto ameishukuru
Kamati ya Utendaji kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ambapo amomba ushirikiano
kwa vyombo ya habari, uongozi na wanachama katika kufanikisha malengo ya
kuifanya klabu ya Yanga kwenda mbele zaidi
on Monday, November 5, 2012
Post a Comment