Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kigong'ota: Ndege Hodari Wa Kutoboa Miti Kwa Mdomo

 


UKO kwenye mbuga ya wanyama – haijalishi kama ni Serengeti, Ngorongoro, Mikumi, Manyara au Selous - mazingira yote yametulia ukifurahia mandhari ya asili na upepo mwanana uliosheheni harufu nzuri.
Waweza kuwa peke yako, wawili au hata wengi, lakini pengine lengo lenu ni kuyasawiri mazingira hayo tuliyojaaliwa na Muumba wetu ambayo hatuyalipii hata ushuru ili yaendelee kushamiri zaidi ya kuhitaji matunzo ya asili kwa kuacha kuchoma moto misitu, kuwinda ovyo bila vibali (ujangili) na kadhalika.
Basi, katika pitapita yako, ukiamini kwamba hakuna mtu mwingine ndani ya msitu huo isipokuwa wewe au ninyi pekee, ghafla unasikia sauti ndani ya msitu, katika miti mikubwa, kama mtu anatoboa miti kwa tindo.
Unashtuka na kustaajabu. Kama una silaha utaikamata barabara na kuanza kunyata kuelekea kule ulikoisikia sauti hiyo. Unaweza kuhisi ni jangili anayewinda wanyama ama anakata miti.
Sauti hii inasikika na kukoma, kama vile mtu anayesikilizia, halafu inaendelea tena. Unapoufikia mti ambao unadhani umeisikia sauti hiyo, ghafla sauti inakoma. Hili linakufadhaisha na unajiandaa ili uweze kumkabili huyo aliye juu ya mti.
Unapoangaza vizuri juu ya mti baada ya sauti kuanza kusikika tena, mara unamwona ndege mmoja mdogo mwenye mdomo uliochongoka ambaye anaendelea kutoboa mti bila hofu yoyote.
Nguvu zote zinakuishia na unabaki kumkodolea macho ndege huyu ambaye ama anaweza kuwa wa kijivu, mwenye madoa meupe na mkia wa njano, huku mdomo wake ukiwa mwekundu.
Ndege huyu anaitwa Kigong'ota, au kwa majina mengine gongonola, gogota, vigotagota au ving'ota na katika sehemu nyingine huko Tanganyika (vijijini zaidi), wanaitwa Nyamkonghona. Ni ndege wa nusu-familia ya Picinaekatika familia ya Picidae, ambaye kwa Kiingereza anaitwa Woodpecker.
Vigong'ota vinatokea misituni na maeneo mengine yenye miti kila mahali pa dunia isipokuwa Madagaska, Australia, New Zealand na kanda za Aktiki na Antaktiki.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top