Na Angetile
Osiah
NYOTA wa
zamani wa Ghana na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa, Abedi Ayew Pele,
amewaambia wachezaji chipukizi wa Tanzania kwamba, hakuna njia ya mkato katika
kutafuta mafanikio na kuwataka kufanya jitihada ili watimize ndoto zao, ikiwa ni
pamoja na Serengeti Boys kuhakikisha inafuzu kucheza fainali za Afrika
mwakani.
Pele, ambaye
aliiongoza Marseille kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya mabao
dhidi ya AC Milan ya Italia, alisema hayo Jana asubuhi wakati alipotembelea Kiti
cha ufundi cha Karume kushuhudia programu ya mazoezi ya vijana wadogo
inayofanyika kila misho wa wiki kwenye Uwanja wa Karume ambako watoto wa kuanzia
umri wa miaka sita hadi 17 hufundishwa mbinu za kusakata
soka.
"Katika
kufikia mafanikio hakuna njia ya mkato," alisema Pele ambaye ameletwa nchini na
Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) kuangalia shughuli
mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
"Tunaona
wachezaji wenye vipaji vikubwa duniani wakifanya jitihada kubwa ili waweze
kucheza kwa kiwango cha juu. Bila ya kufanya juhudi, kujituma na kudhamiria
huwezi kufanikiwa.
"Wale wenye
vipaji vikubwa, lakini hawafanyi jitihada watabakia I. Wale wasiojaliwa kuwa na
vipaji, lakini wanafanya jitihada, watakwenda mbele na kupata mafanikio,"
alisema nyota huyo ww Ghana ambaye alijijengea jina kwa kufunga mabao safi na
muhimu kwa nchi yake na klabu ya Olympique Marseille wakati ikitamba katika soka
barani Ulaya.
"Soka barani
Afrika Lina mazingira yanayofanana. Hakuna motto wa waziri anayecheza soka. Wala
hakuna mtoto wa mwanasheria au mfanyakazi ww benki ambaye anacheza soka. Soka
inachezwa na watu wanaotoka kwenye familia ambazo hazina maisha mazuri na hivyo
man nafasi sawa na wengine wote. Mnachotakiwa kufanya ni kujituma, kudhamiria na
kufanya jitihada ili mfungue mlango wa mafanikio.
Pele, ambaye
jina lake halisi ni Abedi Ayew na ambaye watoto wake wainaichezea Marseille, pia
aliwataka wacheaji aw timu ya Taifa ya Vijana walio na umri china ya miaka 17
kufanya kila wawezalo ili wafuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika
zitakazofanyika Algeria mapema mwakani.
"Mkifuzu
mtakuwa mmefungua milango ya mafanikio ya maisha yenu," alisema gwiji huyo
ambaye anaiwakilisha FIFA katika kufuatilia programu mbalimbali za maendeleo.
"nikiwaangalia naona mna man uwezo wa kuwaondoa wapinzani wenu na nitafuatilia
mechi yenu. Mkifuzu tutakuwa wote na nitawaunga
mkono.
Pele, ambaye
kwa sasa anamiliki shule ya mpira wa miguu ambayo imeshanikiwa kutwaa Kombe la
FA mara moja, ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo wa FIFA kwa nchini za
Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi na mmoja wa viongozi wa Idara ya Mawasiano
ya FIFA, Emmanuel, atakuwa nchini kwa siku tatu ambazo atazitumia kupata taarifa
za shughuli mbalimbali za maendeleo, zikiwemo za soka la watoto (grassroots),
soka la vijana, soka la wanawake na miradi mingine ya
maendeleo.
(Angetile
Osiah ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF)
on Monday, November 5, 2012
Post a Comment