WANAHARAKATI nchini China
wanasema kuwa vijana watatu watawa wa Tibet pamoja na mama mmoja walijiteketeza
mkesha wa kongamano la chama cha tawala cha kikomunisti nchini
China.
Shrika la Free Tibet linasema
kuwa mmoja wa watawa hao alifariki katika kile inachosema ni idadi kubwa ya watu
kujiteketeza kama njia ya kuonyesha kukerwa na utawala wa
china.
Matukio ya hivi
karibuni ya watu kujiteketeza moto katika maeneo ya china yaliyo na watu wa
Tibet yamefikisha idadi ya watu hao wanaojiteketeza kuwa zaidi ya watu sitini
tangu mwaka jana.
Wengi wao
wamefariki. Na huenda kuna umuhimu katika wakati ambapo visa hivi
vimetokea.
Kuimarishwa kwa
usalama kote China kwa kongamano la chama tawala cha kikomyunisti nchini,
hakujazuia malalamiko ya raia wa Tibet dhidi ya utawala wa China. Badala yake
yameongezeka.
Wanaharakati
wanasema idadi ya watu kujiteketeza kwa muda wa siku moja, hii leo,
haikutarajiwa.
Tangu mwaka jana
zaidi ya raia sitini wa Tibet wameamua kutumia njia kubwa kabisa ya kuonyesha
kuvunjwa moyo, kwa kile wanachosema ni ukandamizaji wa China kwa tamaduni
zao.
Maafisa wa
serikali wa China wametoa fedha katika maeneo yaliyo na raia wa Tibet na
wameendelea kukana tuhuma hizo za ukandamizaji.
Mkurugenzi wa
kundi linalotetea kuachiwa huru maeneo ya Tibet, amesema malalamiko ya hivi
karibuni yananuiwa kutoa ishara kwa kizazi kipya cha uongozi China,
kitakachoidhinishwa katika kongamano linaloendelea Beijing, kuwa raia wa Tibet
wataendelea kupigania uhuru wao.
Baadhi ya raia wa
Tibet walio uhamishoni, wanatumai kuwa mwanamume anayedokezwa kuwa kiongozi
mpya, Xi Jinping, huenda akawapatia nafasi ya kufanyika mabadiliko.
Post a Comment