WAZIRI Mkuu Mstaafu , Edward Lowassa, amesema unyonge wa
elimu kwa watoto wa kike hautamalizwa kwa kelele za wanasiasa , bali ni kwa
taifa kuweka misingi imara itayowasaidia kujielimisha kadili ya ukomo wao, ili
wawe na uwezo wa kutosha wa kupambana na changamoto
zinazowakabili.
Kauli hiyo aliitoa jana Jijini hapa, wakati akiendesha
harambe ya kuchangia ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu
cha Teofilo Kisanji (TEKU),kinachomilikiwa na kanisa la MoravianiTanzania (KMT)
na kufanyika katika usharika wa Ruanda jimbo la kusini
Magharibi.
Katika harambe hiyo Lowassa alichangia fedha taslimu
kiasi cha shilingi milioni 25, huku viongozi mbalimbali wa serikali na chama
tawala (CCM) wakiongozwa na na Mkuu wea Mkoa wa Mbeya,Abas Kandoro
aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispine Meela nao wakitoa mchango
wao.
Lowasa alisema ili taifa liweze kujidhatiti kikamilifu ni
lazima watu wake wakaona fursa na kuamua kuwekeza kwenye elimu , ambapo kundi
kubwa la vijana wataweza kujifunza na kuelimika katika mambo
mbalimbali.
Alisema jitihada za kuwakomboa wanawake hususani watoto
wa kike haziishi tu kwa viongozi wa siasa kupiga kelele majukwaani, bali ni
watanzania kuwajengea uwezo wa kila hali ili kuhakikisha wanasoma kwa kadili ya
ukomo wao.
Akizungumzia vijana kwa ujumla Lowassa alisema wanapaswa
kutambua kuwa elimu ndio njia pekee ya wao kujikatika changamoto mbalimbali,
hivyo bila nyenzo hiyo hawawezi kufika mahala popote, badala yake fursa
mbalimbali zitawapita na wao kubaki watazamaji.
“Baba Askofu kwani hata ukitaka kufuga kisasa au
kibiashara lazima uwe na elimu, na hata wale waliojiandaa kufanya kazi za
ofisini wanakuwa na hali ngumu bila kuwa na elimu ya kutosha” alifafanua
Lowassa.
Aliwata vijana kutumia vizuri fursa walizopata za kusoma
katika vyuo vikuu iwe kwa ufadhili wa watu au serikali kwani watu hao
waliowafadhili walijinyima kwa malengo ya kuhakikisha wanawatimizia matakwa yao
ambayo ni faida kwa taifa pia.
Hata hivyo alisema kama vijana wa Tanzania hawataelimika
vya kutosha katika elimu ya juu hawataweza kutoa ushindani wa kutosha kwa wenzao
kwenye soko la ajira kwa nchi za zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Alinikuu kifungu cha Biblia “ Tumeambiwa katika bibilia
takatifu…tusipojibiidisha kutafuta maarifa tutaishia kuwa wateka maji, wakata
kuni kwa wenzenu (Joshua 9:21), kwa hiyo nalipongeza kanisa la Moraviani kwa
bidii na umoja wao kwa kujenga chuo kikuu.”
Aidha, Lowassa aliweka wazi kuwa tabia yake ya kuchangia
katika makanisa ni wito na kamwe yeye si tajiri bali amekuwa ana changiwa na
baadhi ya marafiki zake wanaoshirikiana hivyo kupata fedha hizo ambazo anazitoa
kwenye harambe m,balimbali anazoombwa kuendesha na
kuchangia.
“Mimi naenda sana kwenye harambe sijafirisika, lakini
mimi sio tajiri kama watu wanavyosema ila huwa nachangiwa na wenzangu na hivyo
kuwa na nguvu ya kuchangia kwenye makanisa kama mtakavyoona leo” alisema
Lowassa.
Hata hivyo Lowassa alilipongeza kanisa hilo kwa utulivu
kwa kusema ni tofauti na miaka iliyopita kwa kanisa hilo kuandamwa na migogoro
mingi ambayo ilisababisha kanisa kukosa utulivu na kuwayumbisha waumini
wake.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa kanisa hilo Jimbo la Kusini
Magharibi, Alinikisa Cheyo, katika harambee hiyo lilitarajia kukusanya kiasi cha
shilingi milioni 500 ili kuweza kumalizia ujenzi wa mabweni kwea wanafunzi wa
kike katika chuo hicho.
Na
Moses Ng’wat,Mbeya. picha na mbeya yetu
|
Post a Comment