Dk. Juma Salum Mambi ambae ni Katibu wa Jumuiya
ya Madaktari, akifafanua jambo kwa wajumbe kuhusu katiba yao.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari ZanzĂbar Dk.
Said Mohammed Abdallah akisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na wajumbe
wakati wa mkutano wao uliofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya
Afya.
Madaktari mbalimbali wakimsikiliza kwa makini
Dk. Juma Salum Mambi (hayupo pichani) wakati alipokuwa akijibu maswali yaliyo
ulizwa na wajumbe hao
Dk. Marijani Msafiri akiuliza suali kwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mdaktari Zanzibar Dk. Said Mohammed Abdallah juu ya
suala la kuwa na Mwanasheria wa jumuiya yao katika mkutano wa wanachama
uliofanyika Wizara ya Afya leo.
JUMUIYA ya Madaktari Zanzibar, imefanya mkutano wa kujadili
katiba yake kwa lengo la kuifanyia marekebisho ili iende na wakati wa
sasa.
Miongoni mwa marekebisho hayo,
ni pamoja na kuongeza kipengele cha jumuiya hiyo kuwa na mwanasheria wake.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo
ambaye ndiye aliyeongoza mkutano huo Dk. Said Mohamed Abdullah, aliwashauri
wanachama kuisoma vyema katiba hiyo na kuainisha maeneo wanayohisi yanahitaji
kurekebishwa ili kuiimarisha zaidi .
Alisisitiza umuhimu kwa wanachama kutopuuza
kuhudhuria na kufuatilia vikao kwa lengo la kuwa na jumuiya iliyo imara na
inaweza kusimamia vizuri matarajio yao.
Hata hivyo, wajumbe wote wa jumuiya hiyo
walikubaliana na katiba hiyo, ingawa baadhi yao waliomba wapatiwe muda zaidi wa
kuipitia kwa kina kabla kutoa mapendekezo yao.
Mjumbe mmoja Yussuf Haji, aliwaomba wanachama
wenzake kuiheshimu katiba hiyo, kwani ndio muongozo utakaowezesha kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya hiyo Dk. Juma
Salum Mambi alisema, ili jumuiya hiyo ifanikiwe na na kufanana na jumuiya
nyengine zilizopiga hatua kubwa, ni vyema madaktari wazingatie haja ya kuzidi
kuonesha umoja na mshikamano utakaosaidia kuiimarisha jumuiya
yao.
Mkutano huo umeakhirishwa hadi Disemba 8, mwaka
huu ili kutoa fursa kwa wanachama kuipitia kikamilifu katiba
hiyo.
IMETOLEWA
NA
IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR

Post a Comment