Mjumbe wa Jumuiya ya nchi za visiwa katika bahari ya hindi Raj Mohabeer
(katikati) akizungumza katika mkutano wao na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad nyumbani kwake Mbweni. Kulia ni mjumbe wa
Jumuiya hiyoCorine Paya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza
na Ujumbe wa nchi za visiwa katika bahari ya hindi huko nyumbani kwake Mbweni
Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa jumuiya ya
nchi za visiwa vya bahari ya hindi pamoja na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya
yake.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad amesema Zanzibar inapata manufaa makubwa kutokana na ushirikiano
wake na Jumuiya ya nchi za visiwa katika bahari ya Hindi.
Amesema Serikali inafuatilialia taratibu za kikatiba
ili kuweza kuwa mwanachama kamili wa Umoja
huo.
“Iwapo tutakuwa wanachama kamili, mashirikiano
yatakuwa makubwa na imara zaidi na bila shaka manufaa yataongezeka”, alisema
Maalim Seif.
Maalim Seif alieleza hayo wakati akizungumza na ujumbe
wa Jumuiya ya nchi za visiwa katika bahari ya hindi yenye makamo makuu yake nchi
Mauritius. Mazungumzo hayo yalifanyika nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya Mji
wa Zanzibar.
Amesema Visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na uhaba wa
ardhi kutokana na ongezeko la Idadi ya watu, na kwamba serikali ina mpango wa
kuelekeza ujenzi wa nyumba za ghorofa katika maeneo ya mjini ili kukabiliana na
tatizo hilo la upungufu wa ardhi.
Kwa upande wake mjumbe wa umoja huo Bwana Raj Mohabeer
amesema Zanzibar itaendelea kunufaika na mashirikiano ya nchi za visiwa hata
kama si mwanachama wa umoja huo.
Amesema umoja huo umevutiwa na mazingira ya Zanzibar
na kuelezea matumaini yake kuwa Jumuiya hiyo itakuwa ikifanya mikutano yake hapa
Zanzibar angalau mara moja kwa mwaka.
Nchi hizo za visiwa katika bahari ya Hindi
zinashirikiana katika maeneo tofauti yakiwemo kukabiliana na majanga, mabadiliko
ya tabia nchi pamoja na uhifadhi wa mazingira ya
baharini.
Na
Hassan
Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar
Post a Comment