Rais Banda wa Malawi: Ushoga Ruksa! |
SHERIA ya kukataza ndoa za
jinsia moja nchini Malawi imesitishwa kwa muda mpaka hapo uamuzi utakapotolewa
na Serikali.
Serikali ililiagiza jeshi la
polisi kutowakamata watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja , mpaka hapo
uamuzi utakapotolewa rasmi na Serikali.
Awali Mapenzi ya jinsia moja
nchini Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na
minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.
Baadhi ya viongozi wa
kimagharibi walitishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa
kutambua haki za mashoga
Ushoga ni haramu katika nchi
nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika
zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.
Mmoja wa viongozi wa kijamii
wenye ushawishi mkubwa, Kaomba, aliiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili
sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi
huyo.
Mnamo mwaka 2010, wanaume
wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema
kuwa wataoana.
Kesi hiyo ilivutia sana kero
kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha
msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi
maskini zaidi duniani.
Rais wakati huo akiwa , Bingu
wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa
alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria
za nchi.
Hata hivyo Rais Joyce Banda,
aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na
kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja
Post a Comment