Maneno
yaliyoandikwa kwenye kaburi la kanumba
MIEZI
saba tangu msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba kuiaga dunia Aprili 7,
2012 bado majonzi na vilio vimeendelea kuitikisa familia yake ambapo hivi
karibuni mama yake, Flora Mtegoa na mdogo wake, Seth Bosco waliangua vilio upya
juu ya kaburi lake
Tukio
hilo lilishuhudiwa na paparazi wetu Novemba 4, mwaka huu ambapo mama Kanumba na
Seth walifika katika kaburi alilozikwa Kanumba, Kinondoni, Dar huku wamebeba
maua ikiwa ni mara ya kwanza kulitembelea rasmi kaburi hilo tangu lifanyiwe
ukarabati upya.
“Mimi
sitaacha kumlilia mwanangu Kanumba jamani na siwezi kumsahau maana kifo chake
kilikuwa cha ghafla sana wakati tulikuwa tumepanga mambo mengi.
“Nina muda sijaja kuliona kaburi lake, tangu lilivyojengwa upya sijafika ndiyo leo nakuja huku kwa ajili ya kuliona na kulifanyia usafi. Maskini mwanangu, lala kwa amani baba,” alisema mama huyo huku akilia kwa uchungu ambapo Seth naye alishindwa kujizuia.

chanzo:globalpublishers
Post a Comment