Mtoto wa marehemu Aidan
Libenanga, Aidan Libenanga wa kwanza kushoto akishirikiana na ndugu, jamaa na
marafiki wakiingiza jeneza katika kaburi wakati wa mazishi ya mwandishi huyo wa
habari aliyefariki dunia Nov 18 mwaka huu mkoani Morogoro.
Mzee Aidan Hassan
Libenanga enzi za uhai wake.
Waandishi wa habari
mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani wakiwa na mishumaa wakiwasha kwa ajili ya
kuweka katika kaburi la mpendwa wao Mzee Aidan Libenanga baada ya shughuli za
mazishi kukamilika.
Mke wa marehemu, Aidan
Libenanga, Elizaberth Libenanga 9katikati) akisindikizwa na rafiki zake kuweka
shada la maua katika kaburi la mume wake katika makaburi ya
Kola.
Mbunge wa jimbo la
Morogoro mjini Abdullaziz Abood akitoa heshima za mwisho kwa mwandishi Aidan
Libenanga wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwake kota za Sabasaba Kiwanja cha
Ndege shughuli iliyoanza majira ya saa 7 mchana.
Mwandishi wa IPP MEDIA
mkoa wa Morogoro Devotha Minja naye akitoa heshima zake za
mwisho.
Meya wa Manispaa ya
Morogoro Amiri Nondo naye akitoa heshima hizo.
Ramadhan Libenanga na
kaka yake aliyembeba mtoto wakiaga mwili wa baba yao.
Mratibu wa miradi wa
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) Thadei Hafigwa akiaga
mwili wa marehemu Aidan Libenanga muda mfupi kabla ya kuelekea katika makaburi
ya Kola kwa ajili ya mazishi ya mpendwa wetu.
Mkuu wa wilaya ya
Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka akitoa salamu za uongozi wa mkuu wa mkoa
huo Joel Bendera wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Aidan Libenanga nyumbani
kwake.
Ndugu wa karibu wa Mzee
Aidan Libenanga wakiangua kilio mara baada ya kuaga mwili wa mpendwa
wao.
Mmoja wa watoto wa Mzee
Libenanga akiwa ameshikwa na ndugu kuelekea katika gari kwa ajili ya kwenda
makaburini.
Ni huzuni na vilio kwa
ndugu, jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili wa Mzee
Libenanga.
Post a Comment