Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MANDELA APEWA HESHIMA MPYA AFRIKA KUSINI


THE UNVEILS NEW MANDELA BANK NOTES.Winnie Madikizela-Mandela and Gill Marcus,(middle) the governor of the South African Reserve Bank at the launch of a campaign on 5 September 2012 in Pretoria, the capital on a new range of banknotes honouring former president Nelson Mandela. Photo courtesy Christine Vermooten
The new 10, 20, 50, 100 and 200 rand banknotes feature Mandela’s image on one side and the other side maintains the Big Five animals already on the bills.
 



Noti mpya zenye sura ya Mandela

 
Noti za kwanza zilizo na uso wa rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, zimeanza kutumika nchini humo.
Ni noti za kwanza za Afrika Kusini kuwa na uso wa kiongozi mweusi na zinachukua mahala pa noti zilizokuwa na nyuso za wanyama na picha za viwanda.

Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma anasema kuwa noti hizo zilikuwa kama ishara ya shukrani kwa Mandela.
Bwana Mandela, mweye umri wa miaka 94, ni mmoja wa watu wanaoenziwa sana duniani baada ya kufungwa jela miaka 27 alipokuwa anapigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Gavana wa benki kuu Gill Marcus alikuwa wa kwanza kutumia noti hiyo kwa kununua bidhaa katika duka moja mjini Pretoria.
Alisema kuwa bwana Mandela ana furaha kuona noti hiyo.
Pia alielezea kuwa Afrika Kusini hujaribu kila baada ya miaka saba kubadili sarafu yake ya noti kwa sababu za kiusalama.
Sura ya Mandela iko upande mmoja wa noti hizo mpya wakati wanyama wakubwa watano Simba, Kifaru, Chui , Ndovu na Nyati, wakiwa upande wa pili.
Alishinda tuzo la amani la Nobel mwaka 1993 kwa sababu ya harakati zake dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na kuchaguliwa rais mwaka uliofuata kabla ya kujiondoa mwenyewe mamlakani baada ya kipindi kimoja tu cha utawala wake.
Akisifika sana kwa jina lake "Madiba", amestaafu kutoka kwenye ulingo wa siasa.

CHANZO: BBC SWAHILI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top