Mshambuliaji wa Klabu ya Simba Emmanuel Okwi katikati
akitafuta mbinu ya kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar, Jamali Simba kulia na
Hussein Ramadhani kushoto wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwenye
uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar ilishinda bao
2-0.
KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOTOA KICHAPO KWA
KUITANDIKA SIMBABAO 2-0 KATIKA LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA JAMHURI
MOROGORO.
KIKOSI CHA SIMBA KILICHOTANDIKWA BAO 2-0 NA MTIBWA
SUGAR LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
Benchi la ufundi la klabu ya Mtibwa Sugar likiongozwa
na kocha mkuu wa klabu hiyo Meck Mexime kulia muda mfupi kabla ya vijana yake kuiadhibu Simba
kwa kuwapakipigo cha bao 2-0 katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kutoka kwa
Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Benchi la ufundi la klabu ya Simba likiongozwa na
kocha mkuu Milovan
Cirkovic kushoto muda mfupi kabla ya timu yake kupokea kipigo cha bao 2-0 katika
ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri
mkoani Morogoro
Sehemu ya jukwaa la wazi la mashabiki mchanganyiko nao
wakifuatilia mchezo huo ambao umeishia kwa Simba kukubali kufungwa bao 2-0 na
Mtibwa Sugar.
Jukwaa la klabua ya Simba wakiwa wanafuatilia mchezo
baina ya timu yao na Mtibwa Sugar baada ya kupokea kipigo cha bao
2-0.
Nahodha wa
Klabu ya Simba Juma Kaseja akiwaongoza wachezaji wenzake kuwasalimia wachezaji
wa Mtibwa Sugar.
Mwamuzi wa kati Judith Gamba kutoka Arusha (mwenye
mpira) akiwaongozawachezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar Manungu Turiana na Simba
katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uwanja wa Jamhuri
Morogoro.
Post a Comment