Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya
kipindi cha Makutano, Magic FM
Mheshimiwa Ndugulile akisikiliza swali toka kwa
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango
Mbunge wa Kigamboni akijibu moja ya maswali aliyoulizwa
na wasikilizaji wa Kipindi cha Makutano.Picha na Makutano
Show-
-
Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile
amesema kamwe hajawahi kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali
alitaka serikali imhakikishie kuwa wananchi wanashirikishwa katika
hatua ya maamuzi juu ya mradi wao. Mheshimiwa Ndugulile ameyasema
hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu ya mradi huo katika kipindi
cha Makutano, Magic FM.
Mradi huo ambao sasa ni miaka minne tangu
uanze kuongelewa umezua mjadala mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe
Ndugulile akitolewa kwenye moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano
kutokana na msimamo wake juu ya mradi huo. Alisema tatizo la serikali imekuwa
haitaki kufuata sheria inayotaka ushirikishwaji wa wananchi kila
hatua katika sera ya mipango miji. Pia aliongezea kusema wananchi wanataka
majibu kuhusu lini mradi utaanza, wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu
fidia. Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro
uliojitokeza baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao
kutembelea moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe
Anna Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja ameshajua
kosa lake.
chanzo;;haki
ngowi.com
Post a Comment