Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akitoa
kauli ya serikali Bungeni mjini Dodoma leo juu ya mkakati wa kuondoa uhaba wa
maji jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mh. John Mnyika
akihoji kauli ya serikali bungeni leo.
Serikali imetaja mikakati ya kuondoa uhaba wa
maji katika jiji la Dar es Salaam wakati akitoa kauli ya serikali bungeni mjini
Dodoma leo asubuhi.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe alitaja
baadhi ya mikakati ni pamoja na kupanua na kujenga miundombinu ya
kuzalisha,kuhifadhi na kusambaza majisafi.
Mengine ni kupanua na kuboresha mfumo wa
uondoaji wa majitaka na kuimarisha usimamizi nan utoaji wa huduma ya maji
katika jiji la Dar es Salaam.
Profesa Maghembe pia alitaja mikakati mingine
kuwa pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuongeza fedha za ndani katika
kuboresha usambazaji
Hata hivyo kauli hiyo ya serikali ilihojiwa na
Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika aliyedai kuwa baadhi ya masuala
yaliyosemwa hayakuwa sahihi na mengine yalikuwa hayawezi
kutekelezeka.
Mnyika pia alidai kuwa kauli ya serikali
ilikuwa imeteka hoja yake binafsi ya uhaba wa maji iliyowasilishwa kwa Spika
ili ijadiliwe Bungeni.
Post a Comment