Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKAKATI WA UTANGAZAJI UTALII TZ KUZINDULIWA 15/11/2012


Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki anatarajiwa kuzindua mkakati wa utangazaji utalii wa kimataifa tarehe 15/11/2012 katika hoteli ya Serena hapa jijini Dar es salaam.
Mkakati huo unaotarajiwa kuwa ndio dira ya kuitangaza Tanzania kama eneo la utalii duniani umetengenezwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) linajumuisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii hapa nchini.
Hafla hiyo itakayofanyika kuanzia saa 12.30 jioni itahudhuriwa pia na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi, Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Milao na viongozi wengine kutoka Wizarani. Aidha viongozi wa Shirikisho la vyama vya utalii nchini TCT na wadau wengine wa sekta ya utalii watahudhuria pia hafla hiyo.
Download Our App

1 comments:

Safi saana! Pia wasisahau kuhamasisha utalii wa ndani. Ikiwezekana itengwe siku maalum ya kitaifa ya utalii,ambapo,makampuni na mashirika ya kiserikali au ya binafsi,yatawawezesha wafanyakazi wao kutembelea vivutio vyetu. Au iwekwe sheria kwa kila sekta binafsi au ya kiserikali,kutenga siku yao ya utalii,ambayo itaitwa WIKI YA UTALII kwa kila mwaka walau mara moja,ili wafanyakazi wapate fursa ya kutembelea urithi wao ndani ya nchi. Tusije kujikuta wageni wanafaidika na nchi yetu,hali sisi tumelala. Kwani wao wanapata muda wao vipi kuja kwetu??? Hawana kazi??? Basi kama wanaweza kuacha kazi zao na kuja kwetu, hatuna budi na sisi kutenga muda kwa ajili ya utalii!!
HAYO NDIYO MAONI YANGU!!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top