Dude jipya alilonunua Ronaldo, McLaren MP4-12C Spyder |
|
Ronaldo akiwa katika mitaa ya kwao mjini Lisbon, Ureno juzi, Oktoba 8, 2012. |
Cristiano Ronaldo akiendesha gari lake aina ya Lamborghini Aventador LP700-4 |
Ronaldo akiingia ndani ya gari lake aina ya Lamborghini Aventador LP700-4. |
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejawa na furaha tele kutokana na kiwango cha juu alichoanza nacho msimu huu na kuamua kujipongeza kwa kujinunulia gari dogo jipya la kifahari kwa ajili ya kutanulia mitaani.
Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh. milioni 415).
Sifa mojawapo kubwa ya gari hilo la kisasa ni kasi yake ya kuchanganya mwendo kwani linapowashwa tu, huwa na uwezo wa kufikia spidi ya kilomita 100 kwa saa baada ya muda mfupi wa sekunde 3.1.
Ronaldo alionekana juzi katika maeneo ya kwao, Lisbon nchini Ureno ambako amekwenda kuungana na wenzake katika kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.
Mbali na gari hilo jipya (McLaren MP4-12C Spyder) Ronaldo pia anamiliki magari kadhaa ya kifahari likiwamo aina ya Lamborghini Aventador LP700-4.
Post a Comment