Monalisa |
Udanganyifu
kuhusu maisha halisi ya wasanii wa bongo movie unaweza kuwa unawapa heshima ya
juu mbele ya macho ya watu lakini kumbe inawaumiza indirectly.
The bongo
movie actress ambae ni mkongwe na anayefunika anaposikia Director kasema
‘action’ amefunguka kile ambacho wanakutana nacho wasanii wa bongo movie ambao
wanadanganya kuhusu maisha yao halisi.
Kwa mujibu
wa mtandao wa wajanja club, Yvonne Cherry a.k.a
Monalisa amesema baadhi ya wasanii wa filamu nchini Tanzania
wanadanganya sana kuhusu hali halisi ya maisha yao hasa wanapopata nafasi ya
kuongea na vyombo vya habari kuhusu maisha yao.
“mtu akipata
nafasi ya kuongea na vyombo vya habari kuhusu malipo na maisha yake halisi
utakuta akisema kuwa yeye bila kulipwa milioni tano hawezi kushiriki katika
filamu, lakini ukweli hakuna msanii wa kawaida anayeilipwa fedha kama hizo
katika tasnia ya filamu Bongo, mimi mwenyewe ni mtayarishaji.” She opened
up.
Muigizaji
huyo ambae aliing’arisha filamu ya ‘Girlfriend’ enzi hizo na akina G.K
aliendelea kufunguka kuwa kutokana na udananyifu huo serikali kupitia Bodi ya
filamu iliamua kuongeza gharama za kibali cha kurekodi filamu hadi kufikia
shilingi 500,000 jambo linalofanya wasanii walalamike kuwa ni kiwango kikubwa
sana ukilinganisha na malipo ya filamu. Na kwamba hali ya soko la filamu ni
mbaya kwa sasa.
Ndo hivyo
kumbe!!! Tuendelee kutafakari about our favourites actors and actresses na bongo
movie na hao baadhi ambao wanaigiza hadi kwenye maisha ya ukweli mbele ya
waandishi wa habari.
Post a Comment