![]() |
Haruna Niyonzima anakwenda El Merreikh |
Na Mahmoud
Zubeiry
KLABU ya
Yanga imepokea ofa kutoka klabu mbili tofauti, moja ya Asia na moja ya hapa hapa
Afrika zikiwahitaji wachezaji wao mahiri wa kigeni, kiungo Haruna Niyonzima
kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu kutoka
Burundi.
Habari za
ndani kutoka Yanga, zimesema kwamba, Niyonzima anatakiwa na klabu ya El Merreikh
ya Sudan, wakati Kavumbangu anatakiwa na klabu moja ya Qatar.
Tayari barua
rasmi za kuwahitaji wachezaji hao zimekwishawasilishwa Yanga na hivi sasa klabu
inaingia kwenye majadiliano ya bei na klabu hizo.
Klabu ya
Qatar, ilitangaza ofa ya dola za Kimarekani 100,000 (zaidi ya Sh. Milioni 150),
lakini Yanga imekataa dau hilo na inataka dola 300,000 (zaidi ya Sh. Milioni
450) kwa ajili ya Kavumbangu.
Kuhusu
Niyonzima, Merreikh imeomba itajiwe bei ya mchezaji huyo na Yanga. “Merreikh
wana fedha, hatuna wasiwasi nao, sisi tutaanzia dola 300,000 na hata tukishuka,
si chini ya 200,000, hawa wachezaji ni lulu”kilisema chanzo kutoka
Yanga.
![]() |
Didier Kavumbangu anakwenda Qatar |
Haruna
alisajiliwa msimu uliopita Yanga kutoka APR ya Rwanda, wakati Kavumbangu
amesajiliwa msimu huu kutoka Atletico Olympic ya
Burundi.
Kavumbangu
kwa sasa ndiye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
akiwa ametikisa nyavu mara nane, sawa na Kipre Tcheche wa Azam
FC.
Wataalamu wa
usajili wa Yanga, Seif Ahmad ‘Magari’ na Abdallah Ahmad ‘Bin Kleb’ tayari
wanajiandaa kwenda Kampala, Uganda itakapofanyika michuano ya Kombe la Challenge
kutafuta wachezaji wa kuziba nafasi za Kavumbangu na
Niyonzima.
Lakini
habari zaidi zinasema nafasi ya Niyonzima itazibwa na Kabange Twite kutoka APR
ya Rwanda, ndugu wa mchezaji mwingine wa Yanga, Mbuyu Twite
Post a Comment