Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa ya Ruvuma (FARU) na Njombe (NJOREFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika Novemba 4 mwaka huu.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa FARU na ule wa NJOREFA walivyo na imani kubwa kwao
katikakusimamia mchezo huo katika mikoa yao.
TFF inaahidi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa kamati za utendaji za NJOREFA na FARU zilizochaguliwa
chini ya uenyekiti wa Stanley Lugenge (NJOREFA) na Golden Sanga
(FARU).
Uongozi huo mpya wa vyama
hivyo una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za
mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba za vyama vyao pamoja na vyombo vya mpira wa
miguu vilivyo juu yao.
Pia tunatoa pongezi kwa
kamati za uchaguzi za FARU na NJOREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa
kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama
wa TFF.
Viongozi waliochaguliwa
kuongoza FARU ni Golden Sanga (Mwenyekiti), Dk. Kiyo (Makamu Mwenyekiti), Ahmed
Chale (Katibu), Aljaba Chitete (Katibu Msaidizi), Humphrey Milanzi (Mjumbe wa
Mkutano Mkuu TFF), James Mhagama (Mwakilishi wa Klabu TFF) wakati wajumbe ni
Kevin Haule na Emmanuel Kamba.
Post a Comment