Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize, anaripotiwa
kuchukua hatua isiyo ya kawaida ya kuamrisha mwanawe mwenyewe wa kiume afungwe,
kwa sababu hakulipa bili kubwa ya hoteli.
Afisa wa polisi alisema mtoto huyo wa Rais Bozize, Kevin, anadaiwa zaidi ya dola 13,000 baada ya kukaa kwa siku kadha kwenye hoteli ya fahari katika mji mkuu, Bangui.
Kevin Bozize ni kepteni kwenye jeshi la nchi hiyo.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment