Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonyesha kuwa idadi ya watu wapya walioambukizwa virusi vya ukimwi imepungua kwa asilimia 22 kati ya mwaka 2001 na 2011.
Ripoti hiyo ambayo ilifanyiwa uchunguzi na Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukimwi na HIV, imegundua kuwa idadi ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa ukimwi imepungua katika miaka kumi iliyopita.
Ripoti hiyo imesema kuwa matokeo hayo ni kwa upande fulani kutokana na upatikanaji kwa wingi wa dawa za kuzuia watu walioambukizwa virusi vya ukimwi, lakini imesema pia kuwa kazi kubwa zaidi inapaswa kufanywa.
Mwaka jana lengo lilikuwa kupunguza kwa nusu idadi ya maambukizi ya kila mwaka ya HIV ifikapo mwaka 2015.