Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa
‘Education for All Global Report’ ya mwaka 2012 inayoandaliwa na UNESCO kila
mwaka, ambapo pamoja mambo mengi aliyoyazungumzia pia amesema tukiwa tumebakiwa
na si zaidi ya miaka mitatu kufikia mwaka 2015, michakato ya kutimiza Malengo ya
Maendeleo ya Millenia (MDGs) na Malengo ya ‘Elimu Kwa Wote’ (EFA) lazima
irekebishwe.
Ameongeza kuwa japo
Tanzania inakaribia kutimiza lengo namba 2 la MDGs la ‘Elimu ya Msingi kwa Wote
na lengo la Tatu la Usawa wa Kijinsia lakini bado ziko changamoto, akitolea
mfano katika elimu na kusema msisitizo umeelekezwa katika kuongezwa kwa idadi ya
watoto wanaojiunga shule lakini kimsingi kinachotakiwa ni kuweka mkazo kwenye
kiwango cha elimu kinachotolewa.
Mwakilishi wa Shirika la
UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akiwasilisha matokeo ya ripoti ya 10 ya ya
mwaka 2012 ya ‘Education for All Global leo jijini Dar es Salaam inayoitwa
“Putting Education to Work” na kufafanua kuwa takriban vijana milioni 2 nchini
Tanzania hawajamaliza elimu ya msingi na hawana maarifa ya kuwapatia kazi
itakayowapatia kipato cha kujikimu kimaisha.
Amesema matokeo ya ripoti
hiyo yanaonyesha kuwa juhudi za haraka zinahitajika ili kuwekeza katika
kuwapatia vijana elimu haswa wenye miaka kati ya 15 hadi 24 Tanzania na barani
Afrika kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taifa Chama
cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bw. Lwidiko Edward Mhamilawa akizungumza
katika uzinduzi huo na kuitaka Serikali kuangalia upya Sera ya Elimu kwa kuwa
haimwezeshi Mhitimu kuwa na uwezo wa kufanya kazi itakayomwezesha kuendesha
maisha yake na hivyo kuwa moja ya changamoto kubwa inayoongeza idadi ya vijana
wasiona ajira mtaani.
Kamishna wa Elimu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Eustella Bhalalusesa wakati wa uzinduzi wa
ripoti hiyo ambapo amesema Tanzania itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na
mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Sera za Elimu zinaboreshwa ili
kuinua kiwango cha Elimu na kumjenga kijana kuwa na stadi za kukabiliana na
maisha hata kama hakufaulu darasani.
Mwakilishi wa Shirika la
Kazi Duniani nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akisisitiza ili kuboresha
elimu walimu wanahitaji kupewa mafunzo bora, kupatiwa vifaa vya kufundishia na
mtaala wa Elimu kutoka ngazi ya Taifa mpaka ngazi za chini unahitaji kufuatiliwa
na kusimamiwa.
Moderator wakati wa
kuchangia maoni Juu ya Ripoti hiyo Profesa Idrissa Mshoro akitoa tathmini yake
kuhusiana na matokeo ya “Education For All Global Monitoring Report” kabla ya
kutoa nafasi kwa jopo la wataalam waliohudhuria kuendelea na uchambuzi
wao.
Jopo la Wadau wa Kimataifa
wa Elimu wakitathmini Ripoti ya UNESCO ya Mwaka 2012. Kutoka kushoto ni
Moderator Profesa Idrissa Mshoro, Deputy Head of Mission, Head of Development
Cooperation Division Ubalozi wa Sweden B. Maria Van Berlekom, TVET Section Makao
Makuu ya UNESCO Paris Bw. Borhene Chakroun, Senior Technical Advisor, Education
for Employment Bw. Peter Loan na Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania
Bw. Kabeho Solo.
Meneja Mipango wa Ubalozi
wa Shirika la Maendeleo la Itali katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo
katika Ubalozi wa Italia nchini Bw. Daniele Cristian Passalacqua akichangia
maoni juu wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la
UNESCO nchini Tanzania Bi. Vibeke Jensen.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO)
nchini Tanzania Bw. Alexio Musindo.
Pichani Juu na Chini ni
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka Mashirika ya Maendeleo, Mashirika ya Kijamii
na Sekta Binafsi.
Post a Comment