Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SAJUKI NA WASTARA WATINGA BUNGENI




Baada ya kuponywa na maradhi yalimtesa kwa muda mrefu jana msanii maarufu wa filamu nchini Juma Kilowoko 'Sajui' aliibukia bungeni kwa lengo la kuwashukuru wabunge waliochangia kufanikisha matibabu yake India

Sajuki aliongozana na mke wake Wastara Juma ambaye pia ni mmoja wa waigizaji nyota katika tasnia ya filamu nchini

Ujio wa nyota hao ulitangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni
"Ninawaona wageni wa muheshimiwa Amos Makalla, Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, hawa si wengine ni Juma Kilowoko na Wastara Juma" alisema

"Huyu Juma Kilowoko jina lake la kisanii ni , (wabunge walitaja kwa sauti za juu ni Sajuki) aah kumbe mnalijua , amekuja kuwashukuru wabunge kwa kumchangia matibabu yake "alisema Makinda huku akisindikizwa na makofi kutoka kwa wabunge mbalimbali

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top