Sir
Alex Ferguson amesema anasikia fahari kubwa baada ya hapo jana kuanuliwa rasmi
kwa Sanamu yake mbele ya Uwanja wa Klabu ya Manchester United, Old Trafford,
mbele ya Lango Kuu la kuingiliwa Jukwaa liitwalo Sir Alex
Ferguson.
Uamuzi
wa kuunda Sanamu ya Shaba yenye Urefu wa Futi 9 ulichukuliwa Novemba Mwaka 2011
mara baada ya Ferguson kutimiza Miaka 25 ya utumishi kama Meneja wa Manchester
United kazi ambayo aliianza rasmi tarehe 6 Novemba 1986.
Katika
uanuzi huo, Mastaa wa zamani wa Man United, kina Eric Cantona, Ruud van
Nistelrooy, Ole Gunnar Solskjaer, Edwin van der Sar, Peter Schmeichel, Andy
Cole, Dwight Yorke, Bryan Robson na Ndugu Gary na Phil Neville walijumuika na
Wachezaji wa sasa pamoja na Mashabiki wengi huku David Beckham na Cristiano
Ronaldo wakituma ujumbe uliorekodiwa na kuonyeshwa.
Ferguson,
Miaka 70, alitoa shukrani zake kwa Klabu na Wachezaji wote kwa kumfikisha hapo
alipo na alisema: “Wangetengeneza Sanamu za Wachezaji wote kwa sababu wao ndio
waliotupa mafanikio. Kutoka Mwaka 1986, Wachezaji wametuletea raha
kubwa!”
MATAJI
ALIYOTWAA FERGUSON:
-LIGI
KUU ENGLAND 12 - 92-93, 94-94, 95-96, 96-97, 98-99, 99-00, 00-01, 02-03, 06-07,
07-08, 08-09, 10-11.
-UEFA
CHAMPIONZ LIGI 2 - 98-99, 07-08
-European
Cup Winners' Cup 1 - 90-91
-UEFA
Super Cup 1 - 1991
-FIFA
Intercontinental Cup 1 - 1999
-FIFA
Club World Cup 1 - 2008
-FA
Cup 5 - 89-90, 93-94, 95-96, 98-99, 0304
-LIGI
Cup 4 - 9192, 05-06, 08-09, 09-10
-NGAO
ya JAMII 10 - 90, 93, 94, 96, 97, 03, 07, 08, 10,11
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Man United David Gill alimwelezea Ferguson: "Watu
watasema vitu vingi kuhusu kuwapandishia Wachezaji [Maarufu ikiitwa ‘Hairdryer’]
na Fergie Taimu lakini kitu muhimu ulicholeta kwenye Klabu hii ni kuirudishia
tena heshima yake!."
David
Gill, akiulizwa ni kwanini Mke wa Ferguson, Lady Cathy, ndie aliechaguliwa
kuianua Sanamu hiyo, alijibu: “Yeye ndio sapota mkubwa wa Sir Alex na, nadhani,
Ferguson anamwogopa kidogo!”
Ferguson
alimshukuru Mkewe kwa kumsapoti katika maisha yao yote na akatania: "Cathy
ameahidi kila Jumamosi asubuhi atakuja hapa na kuipigia goti hii
Sanamu!!"
David
Beckham, mmoja wa Wachezaji wa zamani wa Man United, alituma ujumbe uliorekodiwa
kwa Ferguson na alisema: “Ni Siku ya kustajabisha kwako, Familia yako na Klabu.
Napenda niseme asante sana kwa yale yote uliyonifanyia mie! Wakati wangu
nilipokuwa Man United ndio wakati bora kabisa!”
Ronaldo
wa Real Madrid, kwenye ujumbe uliorekodiwa kwa Ferguson, alisema: “Hongera Bosi!
Unastahili kwa Asilimia Mia Moja!”
Straika
wa zamani wa Man United na Netherlands, Van Nistelrool, alisema: “Yote
yanayosemwa hapa hayawezi kulinganishwa na mafanikio aliyopata ambayo
hayasemeki. Ni Mtu mwenye Dira ya kuona mbali, anaweza kujenga Timu upya na hilo
amefanya mara nyingi katika Miaka yake 26.”
Nahodha
wa zamani wa Man United na England Bryan Robson alisema: “Ukipata heshima kama
hii kutoka Klabu kubwa kama Manchester United basi ni lazima umepata mafanikio
makubwa na umepata vitu zaidi kupita Watu wanavyoweza
kufikiria!”
Kipa
wa zamani wa Man United, Peter Schmeichel, alitamka: “Anastahili. Sidhani kama
kuna Mtu hata mmoja humu Nchini na katika Dunia ya Soka ambae ameweza
kusababisha mafanikio makubwa kwa Klabu kama yeye!”
Straika
wa zamani wa Man United na England Andy Cole alisema: “Ni Mtu wa kustajabisha,
Ni Meneja wa ajabu na ndio maana Watu wengi na Wachezaji wengi wa zamani
wamekuja hapa!”
Post a Comment