Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Ndege la Precision, Alfonse Kioko (Kushoto) akipokea funguo za ndege
mpya ya shirika hilo ya ATR 42-600 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Ndege ya ATR Filippo Bagnato (kulia) wakati wa makabidhiano ya ndege hiyo
yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo Bagnato (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Precision Alfonse Kioko (kulia) sehemu mbali mbali kwenye
ndege mpya ya Kampuni hiyo aina ya ATR 42-600 wakati wa makabidhiano ya ndege
hiyo yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo Bagnato (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Precision Alfonse Kioko (kulia) sehemu ya rubani kwenye
ndege mpya ya Kampuni hiyo aina ya ATR 42-600 wakati wa makabidhiano ya ndege
hiyo yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa
wiki. Picha na mpiga picha wetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Ndege la Precision, Alfonse Kioko (wa kwanza) na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuani ya Ndege ya ATR Filippo Bagnato wakishuka kwenye ndege ATR 42-600
baada ya kuifanyia ukaguzi kabla ya makabidhiano rasmi ya ndege hiyo
yaliyofanyika katika kituo cha ATR jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Ndege la Precision Air, Alfonse Kioko (kushoto) akipokea zawadi
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya ATR Filippo Bagnato
(kulia) wakati wa makabidhiano ya ndege hiyo yaliyofanyika katika kituo cha ATR
jijini Toulouse, Ufaransa mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha
Wetu)
********************
Na Mwandishi Wetu,
Toulouse
SHIRIKA la Ndege la
Precision Air limekuwa shirika la kwanza kwenye bara ya Afrika na dunia kwa
ujumla kumiliki ndege ya kisasa aina ya ATR 42-600 baada ya kukamilisha
mchakato wa kununua ndege hiyo jana , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ndege
ya ATR iliyopo jijini Toulouse , Ufaransa Filippo Bagnato
amesema.
Ndege hiyo yenye thamani ya
dola za kimarekani 16.4 milioni (Takribani shilingi bilioni 26.24) ni ndege bora
katika sekta ya usafiri wa anga duniani na inazingatia usalama wa abiria kwa
hali ya juu pamoja na kutoa aina mbali mbali za burudani kwa abiria
wanaosafiri.
Akizungumza wakati wa hafla
ya kukabidhiwa ndege hiyo kwenye kiwanda cha ndege aina ya ATR kilichopo jijini
Toulouse, Ufaransa, mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air
Alfonse Kioko alisema kuwa shirika lake litawekeza zaidi ya dola za kimarekani
milioni 100 kuongeza uwezo pamoja na kutanua safari za shirika hilo katika
kipindi cha miaka michache ijayo.
Kioko alisema kuwa ndege
hiyo mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 iitatumika kupanua safari ya shirika
hilo ya Dar es Salaam – Kilimanjaro na kuongeza kuwa safari hizo zitaanza rasmi
ndani ya wiki mbili zijazo baada kuwasili kwa ndege jijini Dar es Salaam wiki
hii.
“Uwekezaji wa dola milioni
100 utatuwezesha kuwa na jumla ya ndege mpya tano (nne zikiwa ni ATR 42-600 na
moja ikiwa ni ATR 72-600 pamoja na injini moja mpya ya dharura) katika kipindi
cha miaka mitatu ijayo. Ujio wa ndege hizi utaongeza idadi ya ndege zetu za ATR
kufikia 14 na kutuwezesha kutoa huduma bora zenye uhakika,” alisema
Kioko.
Awali Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya ATR Filippo Bagnato alisema kuwa Tanzania itaendelea kuwa soko
muhimu la kampuni yake na kuongeza kuwa atafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa
mahusiano baina nchi hizo yanaendelea kuimarika.
“Utoaji wa ndege ya kwanza
ya ATR 42-600 kwa Shirika la Precision ni swaala la kihistoria katika bara la
Afrika na duniani. Baada ya kukabidi ndege hii Shirika la Ndege la Precision
litakuwa miongoni mwa mashirika mengine yanayotoa huduma bora na zenye
uhakika.
“Kwa kutumia ATR 42-600,
Shirika la Precision itaendelea kujitanua kibiashara na kukumbana na changamoto
zilizopo katika sekta ya usafiri wa anga Afrika na kutoa huduma zenye gharama
nafuu,” alisema.
Kwa upande wake Afisa Mkuu
wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Abubakar Kiroge wakati
wa tukio hilo alisema kuwa uchunguzi katika ndege hiyo umeshakamilika na
kuongeza kuwa ndege hiyo inakidhi vigezo na taratibu zote zinazotakiwa nchini
Tanzania.
“Ndege hii imekidhi vigezo
vya kiusalama vinavyotakiwa. Mamlaka husika sasa ipo tayari kuipatia Precision
Air cheti cha kuwezesha ndege hiyo kutumika nchini Tanzania. Ukweli ni kwamba
ndege hii inazingatia usalama wa abiria kwa haki ya juu,” alisema
Post a Comment