KLABU ya
Manchester United sasa imekaa mkao wa kula baada ya Wesley Sneijder kuambiwa
hawezi kucheza Inter Milan tena hadi akubali kupunguziwa mshahara wake wa pauni
200,000 kwa wiki.
Kiungo huyo
Mholanzi, amegoma kupunguziwa mshahara Inter na Mkurugenzi wa klabu hiyo, Marco
Branca amesema hatahusishwa kwenye mipango ya klabu hiyo akubali kupunguziwa
mshahara.
Sneijder,
ambaye aliiongoza Inter chini ya kocha Jose Mourinho kutwaa taji la Ligi ya
Mabingwa na ya nyumbani mwaka 2010, alikuwa anatakiwa na klabu kadhaa ikiwemo
Man United, lakini Sir Alex Ferguson aliamua kuachana naye kutokana na mshahara
mkubwa alioutaka.
Wesley
Sneijder
Lakini sasa
kuna uwezekano Mholanzi huyo akatua United January.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28, alisaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye
mshahara huo mnono wa pauni 200,000 kwa wiki mwaka 2010, lakini Inter hivi sasa
iko katika mpango wa kupunguza bajeti yake na matokeo yake ni pamoja na kumuuzaa
kipa Julio Cesar kwenda QPR msimu huu.
Branca
ametoa taarifa kuhusu Sneijder, ambaye ametemwa kwenye kikosi kinachomenyana na
Parma leo, katika tovuti ya klabu hiyo.


Post a Comment