Brigedia general Hassan
Ngilizi mwenekiti aliyekuwa anaongoza uchunguzi..
Spika wa Bunge Anna
Makinda Wakati akisoma taarifa hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma..
Mh sara Msafiri
aliyekuwa anatuhumiwa.Amekutwa hana hatia katika ripoti hiyo..
Mbunge wa Simanjiro
Christopher Ole Sendeka alituhumiwa lakini nae hana
hatia.
Mh Maswi Katibu mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Amepewa Onyo kali na spika wa Bunge la
tanzania..
Waziri wa Nishati na
Madini Mh Profesa Sospeter Muhongo nayea ameagizwa kuwa muangalifu katika hotuba
zake kwa kuwa ni muwakilishi wa serikali..
Mh Tundu Lisu ambaye
aliongea na waandishi wa habari na kuwatuhumu baadhi ya bunge naye amepewa onyo
kali na spika wa bunge la tanzania..
Mheshimiwa John Mnyika
mbunge wa ubungo na msemaji wa kambi ya upinzani bungeni ambaye nae katika
hotuba yake aliwatuhumu baadhi ya wabunge nae amepewa onyo
kali..
Mh selasini mbunge wa
Rombo nae alisimama bungeni wakati akichangia hoja ya bugeti ya nishati na
madina nae amepewa onyo kali na spika wa bunge la tanzania..
Sehemu ya taarifa
hiyo...
Maswi aliwatuhumu moja kwa
moja baadhi ya wabunge kwa maandishi kutaka rushwa na wakimtishia kupoteza
nafasi yake ya Ukatibu wa Wizara
- Tume inasema Maswi alitoa tuhuma hizi kwa
lengo la kujihami juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili
- Tuhuma za kuwa Maswi aliombwa rushwa ya
Milioni 50 na wabunge nazo zimetupiliwa mbali kuwa lengo ni kutaka
kujihami.
- Mbunge Selasini alipohojiwa na Tume, alikiri
kuwa hakuwa na ushahidi wa maneno 'aliyoropoka' bungeni akiwatuhumu baadhi ya
wabunge waliohisiwa kupokea rushwa.
- Mnyika alipohojiwa juu ya
kauli yake Bungeni kuwa Maswi anashinikizwa ajiuzulu nafasi yake, Mnyikaalitumia
ushahidi wa vyombo mbalimbali vya habari! Anadai kuwa hakukuwa na kanusho la
habari hizo (labda ndilo lilimpelekea kuamini ni habari
sahihi)
- Ole Sendeka alipohojiwa juu ya kauli yake
bungeni; alidai kuwa alikuwa anajaribu ku pre-empty tu.
- Mbunge Kessy naye alijikanyaga tu kuwa lazima
kulikuwa na rushwa tu
- Waziri Muhongo alipohojiwa na Tume alisema ni
'allegations' tu.
- Mbunge Sarah Msafiri na mwenzake wamesafishwa,
hawakuiuzia TANESCO matairi! Tuhuma za Tundu Lissu pia zimeonekana kukosa
mashiko na amekiri kuwa alipata taarifa toka kwa watu wa Wizara, hakuwa na
ushahidi wa moja kwa moja!
- Wabunge waliotoa tuhuma bungeni, wamekemewa na
kutakiwa kutorudia tena.
- Lissu amekaripiwa vikali kwa kuwachafua
wabunge na waliochafuliwa wameombwa wamsamehe bure.
- Waziri Sospeter Muhongo amekaripiwa kwa
kuwachafua wabunge na ametakiwa awe mwangalifu anapotoa kauli yoyote
bungeni kwakuwa kauli yake inachukuliwa ni kauli ya Serikali
Post a Comment