Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAMASHA LA ASANTE TANZANIA IRINGA LAFANA.

 

Sadiki Juma Kilowoko. na Wastara Juma
Sajuki akiimba na Wastara Jukwaani.
                                         ****************
Na SHABANI MWINYIKAYOKA Iringa.
MAELFU ya wakazi wa Manispaa ya Iringa leo wameshiriki katika tamasha maalum la kumchangia msanii wa filamu nchini Sadik Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Tamasha hilo limefanyika katika uwanja wa Samora na kushirikisha wasanii wengi kutoka klabu ya Bongo Movie Unity ya jijini Dar es salaam.

Awali kulikuwa na mechi ya mpira wa Miguu kati ya wasanii hao na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa ambapo wameweza kutoka sare ya mabao 2—2.
.
Sadiki Juma Kilowoko
Sajuki akiwapagawisha wakazi wa Iringa Uwanja wa Samora.
Mohamed Nurdin, Vincent Kigosi, Jimmy Mafuvu,  Hisany Muya
Kikosi kamili cha Timu isiyifungika ya Bongo Movie Club.
Mzee Yusuf, Badra Idabu, Mayasa Mrisho, Maya
Mzee Yusuf akiwazungusha Viuno Bongo Movie Stejini.
Watangazaji wa Iringa
Kikosi makini cha timu ya Watangazaji Iringa katika picha ya pamoja.
Wakazi wa Iringa
Umati uliohudhuria tamasha la Sajuki
Juma Kilowoko
Sajuki akiwa na mkewe Stara wakiimba kwa pamoja.

Akizungumzia tamasha hilo, mke wa Sajuki, Wastara Juma ameelezea kufurahishwa kwake na tamasha hilo na kuwashukuru wadau mbalimbali waliojitolea kulifanikisha huku pia akiwashukuru wasanii na wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kuhudhuria katika tamasha hilo.
Naye Sajuki amewashukuru wananchi wa mkoa wa Iringa na wa Tanzania kwa ujumla kwa kufanikisha tamasha hilo kwa amani na utulivu na amemshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa afya njema siku hadi siku na kuwaomba wadau mbalimbali waendelee kumsaidia kwani bado anahitaji matibabu.
Tamasha hilo lilipambwa na wana-Bongo movie pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva na muziki wa Taarab kama vile Kitale na mfalme wa Taarab nchini na mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf.
Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Iringa wameelezea kufurahishwa kwao na tamasha hilo na kuomba waandaaji waendelee kuwaletea matamasha kama hayo tamasha hilo limeandaliwa na Ibony fm, Clouds Media Group, Glory Lodge likipewa support na wasanii wa filamu kutoka Swahiliwood sambamba na watangazaji wa mkoa wa Iringa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top