Wanasayansi wamemgundua Tembo mmoja wa Asia ambae kwa namna moja au nyingine hutoa sauti za matamshi ya kibinadamu.
Tembo huyo anayeitwa Koshik anaweza kutoa sauti zenye kuashiria maneno tofauti ya lugha tano za Korea.
Sauti anazozitoa zitafsiriwa kwa kiingereza kuwa ni “Hello”, “Good”, “lie Down”, “No” na “Sit Down”.
Tembo huyo amekuwa akirekodiwa katika Zoo moja huko Korea Kusini.
Hata hivyo tembo huyo Koshi anayetua sauti hizo kwa kuingiza mkonga wake mdomoni hadhaniwi kumaanisha anachokisema.
Post a Comment