Naibu Waziri
Mkuu wa Uingereza, Nick Clegg ameonya kwamba wabunge pinzani katika bunge la
nchi hiyo huenda wakaiona Uingereza inajitoa kwenye Umoja wa
Ulaya.
Clegg kiongozi wa chama cha
Kiliberali kinachounga mkono Umoja wa Ulaya ameyatoa matamshi hayo baada ya
Waziri Mkuu David Cameron, kushindwa vibaya bungeni kuhusu mpango wake wa kutaka
kupunguzwa kwa bajeti ya Umoja wa Ulaya.
Cameron amesema atapambana
kuhakikisha matumizi katika bajeti yanapunguzwa. Aidha, anataka bajeti ya muda
mrefu ya Umoja wa Ulaya iongezeke sambamba na mfumuko wa
bei.
Habari hii ni
kwa hisani ya idhaa ya Kiswahili ya DW.
Post a Comment