TAARIFA KWA
UMMA
Uzinduzi wa Shindano la
Kusaka Mabingwa wa Kero kwa Wateja
Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali
nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi
shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini
Tanzania.
Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada
mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa
kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini
Tanzania.
Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza
wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha
umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni
Mfalme.
Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo
kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja
wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya
Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana
kama HUDUMA
BONGO.
Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika
kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter
au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako
utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa
wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote
kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi
katika soko hili la ushindani.
Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma
Bongo - hudumabongo@gmail.com
Novemba 9,
2012
Post a Comment