-Warudishwa tena
Rumande
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Zanzibar
Mahakama ya Wilaya ya MwanakwerekwE ya mjini
Zanzibar, leo imetoa fursa ya dhamana kwa Viongozi wa makundi mawili ya kidini
Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufanya fujo na kupelekea ghasia na vitendo
vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ya
barabara.
Watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maimamu Zanzibar Sheikhe, Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho
Sheikhe, Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid
Hamdan, Khamis Ali Suleiman na Hassan Bakar
Suleiman.
Akisoma uwamuzi huo huku kukiwa na ulinzi mkali
eneo lote la Mahakama, Hakimu wa Makahama hiyo Mh. Msaraka Pinja, amesema kuwa
ingawa upande wa Mashtaka ulikuwa haukutoa pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa,
lakini Mahakama ililazimika kusitisha utoaji dhamana baada ya kupitia mambo
kadhaa ya msingi.
Amesema kuwa pamoja na uzito wa tuhuma
zinazowakabili watuhumiwa, Mahakama ililazimika kusita kutoa dhamana kwanza kwa
usalama wa watuhumiwa wenyewe na kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo
na uwezekano wa kuingilia upelelezi wa kesi
inayowakabili.
Hakimu huyo alisema wasiwasi wa Mahakama
ilikuwa kwamba watuhumiwa hao wakiwa nje ya dhamana kuna uwezekano wa kutenda
kosa lingine, Kutohudhuria Mahakamani kwa wakati wanapotakiwa na kuangalia kwa
mapata uzito wa kosa wanaloshitakiwa nalo.
Baada ya kuridhika na Mahakama hiyo ilitoa
dhamana kwa watuhumiwa wote saba kwa mashariti ya kuwasilisha mahakamani fedha
taslimu kiasi cha shilingi milioni tatu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini
watatu ambao ni watumishi wa Serikali kwa kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha
fedha mahakamani.
Watuhumiwa hao pamoja na Wadhamini wao, kwa
pamoja wametakiwa kuwasilisha barua kutoka kwa Sheha wa Shehiya anayoishi pamoja
na kivuli cha vitambulisho vya Zanzibar Mkazi na kwa wale wenye Hati za
Kusafiria pia wawasilishe vivuli vya hati hizo
Mahakamani.
Pamoja na masharti hayo ya jumla, lakini pia
wadhamini wometakiwa wawe watumishi wa serikali na wawakilishe barua kutoka
katika ofisi wanazozifanyia kazi na vivuli vya vitambulisho vyao vya kazi ili
view kama kumbukumbu mahakamani.
Hata hivyo watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande
baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana pamoja na kukabiliwa na kesi
nyingine Mahakama Kuu ya Vuga, kesi ambayo dhamana yake imewekewa pingamizi kwa
hati maalum ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa sababu za
kiusalama.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi Novemba 21,
mwaka huu itakapotajwa tena.
Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo mmoja ya Mawakili wa Watuhumiwa hao Bw. Abdallah Juma, amesema yeye pamoja
na wakili mwenzake Bw. Salum Toufik, wataendelea kuwatetea watuhumiwa hao hata
baada ya kutishia kujitoa kwenye kesi hiyo mwezi
uliopita.
Post a Comment