* Asema
kuwapa uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi Bucha Fisi
NA
BASHIR NKOROMO, GEITA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katoro
Mazemule na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni 16.5 za
Halmashauri ya kijiji hicho wafikishwe mahakamani haraka.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara leo, katika mji mdogo wa Katoro, mkoani Geita, Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, ni lazima wahusika wote wa wizi
wa fedha hizo wafikishwe mahakamani kwa kuwa ni jasho la
wananchi.
Fedha
hizo zinadaiwa kuliwa na Mwenyekiti huyo kwa tiketi ya Chadema, katika kipindi
cha mwaka 2010 na 2011 hali ambayo imezusha tafrani miongoni mwa wananchi na
uongozi wa Halmashauri ya Kijiji hicho hadi sasa.
Nape
alisema, ni lazima Mwenyekiti huyo na waliohusika wote wafikishwe mahakamani kwa
kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza upotevu wa fedha hizo ilishamaliza kazi yake
na ripoti kukabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.
"Kamati
ya kuchunguza wizi wa fedha hizi ambazo ni mali ya wananchi ilishafanya kazi
yake na kukabidhi ripoti kwa mamlaka zinazohusika, sasa kinachosubiriwa ni nini
wahusika hawa kupelekwa mahakamani?", Nape alihoji na kuongeza;
"Sasa
CCM kwa kuwa ndicho chama tawala, tunaagiza hatua za kuwapeleka mahakamani
wahusika wote zichukuliwe haraka ili haki itendeke".
Nape
alisema, kutotokea kwa wizi wa fedha hizo chini ya uongozi wa Halmashauri ya
Kijiji hicho ambao upo chini ya chama hicho, ni dalili kwamba kujidai kwao kuwa
wasafi na wapigania haki za wanyonge ni sawa na kilio cha
mamba.
" Kila
mara tumekuwa tukiwaambia acheni kuhadaiwa na Chadema, hawa siyo chama cha siasa
ni kundi la wajanja fulani, sasa Wana Katoro mmejionea wenyewe, mmewajaribu
mkawapa halmashauri yenu, fedha wamezitafuna sasa mnahangaika", alisema na
kuongeza;
"Kwa
kuwa mmepata funzo hili, bila shaka hamtaruidia tena, kwani mmeshafahamu kwamba
kuikabidhi uongozi Chadema ni sawa na kumkabidhi fisi bucha".
Mapema,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, alisema kwenye mkutano huo
kwamba, kama hatua za kuwafikisha mahakamani wahusika hazitachukuliwa haraka,
ataongoza wananchi wa Katoro kuandamana ili kuhakikisha hatua hizo
zinachukuliwa.
Kabla ya
mkutano huo, NMape alifungua shina la wajasiriamali la CCM, Bugayambele lenye
wanachama 53 ambao hushughulika na kazi za kutengeza fenicha mbalimbali katika
karakana yao iliyopo eneo hilo la Katoro.
Akifungua
shina hilo, Nape aliahidi kuwapa sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza
shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kununua vitendea kazi kama randa za mbao,
mashine ya kuchetrza mbao na ujenzi wa banda kwa ajili ya shughuli
hizo.


Post a Comment