Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Uanachama wa TPSF, Louis Accaro, alipokuwa akifungua mafunzo ya
fursa za ajira zilizopo kwenye soko la EAC kwa Watanzania wa kada
mbalimbali.
Alisema mkataba wa kuanzishwa kwa soko la pamoja
unatoa fursa za ajira kwa kada mbalimbali kama walimu, madaktari na wahandisi
pamoja na kada nyinginezo hivyo milango iko wazi kuchangamkia ajira hizo.
Alisema “Watanzania wengi hawajui kama wanaweza
kwenda kufanyakazi Kenya, Rwanda ama kwingineko Afrika Mashariki. Tunatoa
mafunzo haya kwa nia ya kuwakumbusha kwamba kuna fursa hizi kwa hiyo walimu,
madaktari na wahandisi waende.”
Alisema wapo Watanzania wachache ambao
wanafanyakazi Botswana na Afrika Kusini, lakini bado hawajaweza kutumia soko la
EAC.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalam wa Kituo cha
Biashara ya Kimataifa (ITC).
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment