MISS Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kabla ya mwaka
2010, alishahusishwa kimapenzi na wanaume kadhaa, akiwemo Khaleed Mohamed ‘TID’,
Hery Samir ‘Mr. Blu’, Jack Pemba, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’, Hartmann
Mbilinyi, Jumbe Yusuf, marehem Steven Kanumba ‘The Great’ na wengineo.
Mtoto mduchu anayefanya Bongo Fleva, Nasib Abdu Juma ‘Diamond’, alianza kung’ara mwaka 2010 pale aliponyakua tuzo tatu za Kili Music Awards na baada ya hapo, alijihesabu kuwa staa, hivyo kula sahani moja na mastaa ambapo sasa matokeo yanaelekea kumfelisha kimuziki.
Jumamosi iliyopita, Diamond alifanya shoo kwenye Fainali za
Miss Tanzania 2012-2013 na jinsi alivyoonesha uwezo mdogo siku hiyo, wadau
walinena kwamba kijana ameanza kufeli kimuziki, ule uhodari wake wa kucheza na
jukwaa umepotea.
WEMA NA DIAMOND |
Diamond akipondwa na kushushwa hadhi, nyuma yake kuna
maneno kuwa chanzo cha uwezo wa dogo huyo kushuka ni mapenzi na mhusika mkuu ni
Wema. Ipo wazi kwamba Diamond na Wema wameshindwa kuachana licha ya kutangaza
kufanya hivyo mara nyingi.
HUU NDIYO MWANZO WA MWISHO WA DIAMOND?
Mwanzo wa mwisho ni msemo kutoka kwenye maneno ya
Kiingereza, The beginning of the end. Hoja ni kwamba kiwango kidogo
alichokionesha Diamond kwenye jukwaa la Miss Tanzania ni ashirio baya kuwa
huenda ndiyo mwanzo wa mwisho wake kutamba kimuziki.
Kilichoonekana siku hiyo ni kwamba Diamond hana jipya na
zaidi ameanza kuwa mzito jukwaani. Amekosa ubinifu wa kumfanya shabiki amuone wa
tofauti. Amebaki yuleyule, hivyo biashara yake inaelekea ukingoni.
Kwa macho rahisi unaweza kutoa kauli kwamba Diamond
amebweteka au amelewa sifa lakini ukweli ubaki kwenye mstari kwake kuwa penzi la
Wema ni kilevi kikali kwake ambacho kwa kasi ya ajabu kinampotezea dira.
Diamond baada ya kulewa mapenzi ya Wema, sasa amegeuka sokomoko au pampula. Na kwa sababu ‘bwa mdogo’ huyo asili yake ni Kigoma, kule mlevi huitwa mboregwa, kwa hiyo binti wa Balozi Isaac Sepetu, amemfanya staa wa wimbo wa Mbagala awe mboregwa wa mapenzi.
Kama zamani alipokuwa anafanya shoo, watu walikuwa hawakai,
wanacheza na kumiminika jukwaani kumtuza, siku hiyo aliimba wapi! Akateremka
kuwafuata mashabiki walipo lakini hakuna aliyesimama wala kuonesha kusisimkwa na
shoo yake. Napigia mstari, this is the
beginning of the Diamond’s end.
Hivi karibuni katika shoo ya Fiesta 2012, Diamond
alishindwa kupokea shangwe zilizozoeleka, hata alipoamua kuvua nguo na kubakisha
ile ya ndani, bado alichemka. Zaidi akaonekana kuharibu zaidi kuliko
kujenga.
Diamond alivua nguo, kipindi ambacho Wema yupo kwenye gumzo
zito kutokana na jinsi ambavyo alikuwa anacheza nusu uchi jukwaani katika shoo
kadhaa za Fiesta 2012. Kwa maana hiyo, Diamond alipovua nguo ilitafsiriwa
amemuiga Wema.
Unapomuiga mtu maana yake unakuwa umemkubali, kwa hiyo
Diamond ‘amechizika’ kwa Wema kiasi ambacho hata uchafu anaoufanya yeye anauiga.
Kwa mantiki hiyo Diamond na Wema ni kama boyfriend kama girlfriend (like a
boyfriend like a girlfriend).
DIAMOND ANAHARIBIKA SI UTANI
Hapati muda wa kufanya mazoezi, anatumia muda mwingi
kujiuguza maradhi ya mapenzi. Hii ndiyo sababu kwamba sikushangaa kumuona
akichemka jukwaani. Wala sijiulizi ni kwa nini kiwango chake kinaporomoka kwa
kasi.
Oktoba 26, 2012 usiku wa kati ya saa 8 na 9, nikiwa naendesha ‘kibebi-woka’ changu nikitokea ofisini kwetu Bamaga, Mwenge, naelekea nyumbani Kijitonyama, nilipofika Mtaa wa Akachube (Kijitonyama), nilimkuta Wema akiwa anaongea na simu huku amezungukwa na watu.
Nikafunga breki, nikashusha kioo nikamsalimia naye akaitika. Nilipoona hayupo kwenye hali ya kawaida nikashuka. Stori niliyoipata pale ni kuwa kumbe alikuwa amegombana na Diamond muda mfupi uliopita.
Eneo la tukio (jirani kabisa na kwa Wema), alikuwepo pia
mwanamuziki Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’. Nilipoona mazingira hayavutii,
nikamuacha Ommy anamtuliza Wema, mimi nikaondoka zangu.
Asubuhi nikaambiwa kuwa Diamond alirudi nyumbani kwa Wema,
suluhu ikapatikana. Jaribu kufikiri kuwa kama mtu usiku wa manane yupo bize na
mapenzi, migogoro isiyokwisha ni saa ngapi atatulia kubuni shoo? Ni muda gani
atautenga kwa ajili ya kutengeneza staili mpya?
JE, ANAYAJUA YALIYOMKUTA KANUMBA KWA WEMA?
Mungu amlaze mahali pema marehemu Kanumba ambaye ndiye
aliyemfanya Wema aingie kwenye ulimwengu wa filamu. Mapenzi yalipokolea, The
Great alilewa kiasi kwamba alishindwa kabisa kustahimili vishindo.
Kwa mara ya kwanza Kanumba aliripotiwa kupigana kwa sababu
ya Wema. Staa huyo wa filamu akawa hatulii, mara yupo polisi kwa sababu ya kesi
ya Wema, ufanisi wake ukaporomoka. Nadhani kuna kitu, sasa namuona Diamond
anashika mkondo uleule.
Kanumba aliposhtuka alimuacha Wema na kuanzia hapo alirudi
kung’ara kwenye soko la filamu.
Wema alimchonganisha Kanumba na Jumbe wakapigana, mwanamke
huyo kawachonganisha Diamond na hasimu wake, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’.
Ikidaiwa kuwa mrembo huyo amempa penzi Bob Junior.
Itaendelea wiki ijayo.
Na Luqman Maloto (Global Publishers)
Post a Comment