YANGA imeendelea kuwapa raha
mashabiki wake, baada ya kufanikiwa kumaliza vema mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara ikijishindilia kileleni zaidi, kufuatia ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.
Yanga imemaliza mzunguko wa kwanza
ikiwa na pointi 29, ikifuatiwa na Azam FC katika nafasi ya pili yenye pointi 24
na Simba SC nafasi ya tatu kwa pointi zao 23.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele
kwa bao 1-0. Lililotiwa kimiani na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Burundi,
Didier Kavumbangu dakika ya 28, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Simon
Msuva.
Kipindi cha pili, Yanga
walirejea na moto wao tena na iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la pili,
mfungaji Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyeuwahi mpira ambao aliuokosa beki wa
Coastal, Mbwana Hamisi na kuutumbukiza
nyavuni kiulaini.
Yanga SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar
Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Nurdin Bakari, Frank Domayo,
Simon Msuva, Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima na Didier Kavumbangu/Said
Bahanuzi.
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail
Amour Khamis, Juma Jabu, Jamal Macherenga/Othman Omar Tamim, Mbwana Hamisi,
Jerry Santo, Soud Mohamed, Razack Khalfan, Daniel Lyanga, Atupele Green/Lameck
Dayton na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Post a Comment