MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya
Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa
taifa.
Kutokana
heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake
katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa
CCM.
Zitto
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum
na Mtandao wa Jamii Forum juzi.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, jana alilithibitishia
gazeti hili kwamba alihojiwa na mtandao huo kwa saa nane.
“Kweli ni
mahojiano baina yangu na Jamii Forum. Kwa Kfupi ni kwamba, yalikuwa mahojiano
ya saa nane, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi jioni na walionihoji kwa njia
ya mtandao walikuwa wakituma maswali na mimi nawajibu,” alisema
Zitto.
Alisema
yeye na Rais Kikwete wana uhusiano nje ya siasa na hata siku moja hawajadili
mambo ya vyama vyao wanapokutana na kwamba, Rais anaamini katika uzalendo
wake.
Zitto
alisema kutokana Rais Kikwete kuthamini mchango wake, ndiyo maana hajawahi
kwenda kwenye jimbo lake kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha CCM katika
chaguzi za mwaka 2005 na 2010.
“Hatuna
makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005
hakuja Kigoma Kaskazini na 2010 pia hakuja Kigoma Kaskazini,”
alisema.
Alisema
kama ilivyo kwa wengine wenye uamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama
vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi
zake.
Aithdha,
Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete kama mzee wake na kwamba, kuwaita kuwa
wao ni marafiki ni kukosea.
“Kuita
sisi ni marafiki ‘is understatement’, yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini
ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania,” Zitto
alisema.
Alichokifanya
Rais Kikwete kutokuja katika jumbo langu si jambo geni, kwani hata vyama vingine
vimewahi kuvifanya.
Alitoa
mfano wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu mwaka
2005, Freeman Mbowe alipofika katika Jimbo la Musoma Mjini, alimpigia kampeni
mgombea wa CUF.



Post a Comment