Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu akimkabidhi nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul
Mgaya kombe la Ubingwa wa michuano ya Uhai Cup 2012 baada ya timu hiyo kuifunga
Coastal Union ya Tanga kwa penalti 3-1 katika mchezo wa fainali ya vijana chini
ya miaka 20 uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Tenga. (Picha na
Habari Msetoto Blog)
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Angetile Osiah akimkabidhi zawadi ya mfungaji bora wa mashindano ya vijana chini
ya miaka 20 ya Uhai Cup, Ramadhani Mkipalamoto wakati wa fainali ya michuano
hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya
kukabidhiwa kombe lao.
Habari na picha na Habari Mseto

Azam Academy wakiwa na Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Abedi pele alipowatembelea Chamazi hivi karibuni |
Na Prince
Akbar wa Bin Zubeiry
TIMU ya
vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam, maarufu kama Azam Academy,
imehitimisha wiki ya furaha kwa klabu hiyo, baada ya kunyakua ubingwa wa Kombe
la Uhai, linaloshirikisha timu za vijana za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara jioni ya leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
Azam Akademy
imetwaa ubingwa huo, baada ya kushinda kwa penalti 3-1, kufuatia sare ya 2-2 na
Coastal Union ya Tanga ndani ya dakika 120 za pambano kali na la
kusisimua.
Ushindi wa
Azam Academy, unakuja siku moja tu baada ya kaka zao, Azam FC kutwaa ubingwa wa
Kombe la Hisani jana mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa
kuwafunga wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya
dakika 90.
Jana Azam
walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha
dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju
miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih
Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Katika
mchezo wa leo, Azam ilimenyana kiume na Coastal ambayo inaonekana kuinukia
vizuri katika uwekezaji kwenye soka ya vijana kabla ya bingwa kupatikana kwa
mikwaju ya penalti.
Mapema
asubuhi katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Simba waliokuwa mabingwa
watetezi, waliifunga 3-0 Mtibwa Sugar na kunyakua nafasi
hiyo.
Aidha,
Bakari Shime wa Coastal Union ametwaa tuzo ya Kocha bora, Mansur A. Mansur wa
Coastal Union kipa bora, Ramadhan wa Simba aliyefunga mabao sita, ameibuka
mfungaji bora, Ruvu Shooting timu yenye Nidhamu, Joseph Kimwaga wa Azam mchezaji
bora na Isiaka Mwalile refa bora.
Post a Comment