'Hailie' mtoto wa Eminem |
Meneja wa Eminem Paul Rosenberg
amekanusha tuhuma kuwa binti wa Eminem Hailie Mathers alimvaa kwa matusi
mwandada Taylor Swift. Meneja huyo amesema Tweet iliyosemekana kuwa ni ya
jumanne, December 4, iliyoaminika kuwa imeandikwa na binti huyo sio ya kweli (ni
fake tweet).
Kwa mujibu wa meneja huyo binti wa
Eminem hana hata account ya twitter. Katika ripoti hiyo aliwaomba radhi fans wa
Eminem na kusistiza kuwa Hailie Mathers hajawahi kujiunga na mtandao wa Twitter
kwa hiyo haiwezekani ikawa katweet kumdiss Taylor Swift.
Mwanzoni ilionekana kuwa kuna mtu ambae
alitumia jina la Hailie ambalo ni jina la mtoto wa kike wa mkali wa michano the
Slim Shade Eminem, na kutweet, “If @tailorswift 13 is really dating the love of
my life @harry styles I will not be happy!.”
Mtu huyo alionesha hisia zake kuwa
hakupenda kabisa uhusiano wa kimapenzi uliochipukia kati ya member wa kundi la
One Direction Harry Styles.
Mtu huyo aliendelea kutweet kumponda
Tailor Swift, “Dear@taylorswif 13, please stop whoring around with every guy you
see. We all know you’re only doing it so you can make another album." The fake
Hailie added, "I am never, ever, everrrrr, listening to your music againnnn,
@taylorswift13. LIKE EVER.”
Post a Comment