Mwenyekiti wa Bodi ya hiyo, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma, aiiiambia NIPASHE jana kuwa walikabidhiwa ripoti ya awali na CAG juzi.
CAG ametukabidhi initial draft (rasimu ya awali) ambayo inaeleza mambo yote ambayo tuliwaagiza wayafanyie kazi kwa maofisa wa Tanesco tuliowasimamisha kazi na nini kilichomo ndani ya ripoti yenyewe, alisema Mboma.
Alisema baada ya kupokea ripoti hiyo ya awali, bodi ilikutana jana kujadili na kwamba wamekubaliana na CAG ripoti kamili iwasilishwe Disemba 28, mwaka huu.
Maafisa hao ambao wanasubiri maamuzi ya Bodi ya Tanesco baadha kukamilika kwa uchunguzi dhidi yao ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Manunuzi Harun Mattambo.
Maafisa hao walisimamishwa kazi tangu Julai 14, mwaka huu na Bodi ya Tanesco. Maafisa hao walisimamishwa sambamba na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, ambaye baadaye alifukuzwa kazi.
Baada ya kusimamishwa kazi kwa maafisa hao, Bodi ya Tanesco ilimpa kazi CAG kuchunguza tuhuma zilizokuwa zinawakabili viongozi hao na CAG alianza uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zinamkabiri Mhando.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wa tuhuma za Mhando, Bodi ya Tanesco ilitangaza kumfukuza kazi rasmi Mhando baada ya kubainika kutenda kosa la kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi.
Hata hivyo, Bodi ilisema kwa kosa alilolifanya Mhando hawezi kushitakiwa mahakamani kwa sababu makosa aliyoyafanya ya kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi ni kosa la kiuadilifu.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment