Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CANNAVARO AREJESHWA STARS, MAKINDA YA SIMBA SC YATEMWA

 



Cannavaro

Na Princess Asia wa Bin Zubeiry
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kung’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mjini Kampala, Uganda.
Katika michuano hiyo, Cannavaro ambaye pia Nahodha wa Zanzibar, aliiongoza timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika michuano iliyoanza Novemba 24 na kufikia tamati Desemba 8, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 24, ndani yake akiwatema chipukizi aliokuwa akiwakomaza kwenye timu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Edward Christopher, wote wa SImba SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen alisema kikosi hicho kitaingia kambini keshokutwa kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo itakayochezwa Desemba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na Cannavaro na Aishi Mangula, nyota wengine wapya walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na Hamisi Mcha ‘Vialli’ na Samir Hajji Nuhu wote wa Azam FC.
Wengine walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam FC), mabeki; Amir Maftah (Simba), Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nasoro Masoud ‘Chollo’ (Simba) na Aggrey Morris wa Azam FC.
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngassa (Simba), Frank Domayo (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athumani Idd ‘Chuji’ (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top