WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku na kuagiza kuondolewa vizuizi vyote vilivyoanzishwa na Halmashauri kwenye stendi za barabara kubwa kwa ajili ya kukusanya ushuru kwani vinaleta usumbufu kwa abiria.
Kauli hiyo ilitolewa waziri
huyo jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofanya ya ziara ya kushtukiza kwenye
Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi majira ya saa 11:30 alfajiri,
ili kujionea utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra), na Kikosi cha Usalama Barabarni (Trafic), haswa katika udhibiti wa
nauli holela katika kipindi hiki cha sikukuu ya Chrismas na mwaka
mpya.
Alisema uwamuzi wake huo
unatokana na kubaini kuwa Halmashauri hizo, zimekuwa zikiwalazimisha madereva
kuingiza magari (Mabasi), kwenye vituo hivyo ambavyo siyo rasmi kwa lengo la
kujikusanyia ushuru.
Amevitaja vituo hivyo
vilivyolalamikiwa kwa usumbufu huo, kuwa ni pamoja na Mafinga, Kibaigwa, Nzega,
Kibaha na vingine.
“Madereva wamekuwa
wakilazimishwa kuingia katika stendi hizi hata kama hawana abiria wakushuka
amakupakia, kitendo ambacho kinawapotezea abiria muda wao wakufika kule
wanakokwenda bila sababu za msingi”alisema Dk Mwakyembe.
Alisema utaratibu huo
haukubaliki, endapo ukiachwa uendelee hivyo iko siku watazuka watu watafikia
hatua ya kuanzisha vizuizi kama hivyo majumbani mwao lengo likiwa ni kuibia
wananchi.
Dk Mwakyembe amezitaka
Halmashauri hizo kuacha utaratibu huo na baadala yake watafute vyanzo vingine
vya ukusanyaji mapato.
Katika hatua nyingine Dk
Mwakyembe amewaonya baadhi polisi wa kikosi cha usalama barabarani kutokana na
mtindo wao wakusimamisha magari kwa kushtukiza wakitokea
vichakani.
Alisema malalamiko hayo
ameyesikia siku nyingi hivyo ameahidi kuwa atayafanyia kazi, ambapo
aliwatahadharisha askari wenye tabia kama hizo, watambuwe muda wao sasa
unahesabika.
Akizungumzia hali ya
usafiri katika kipindi hiki cha sikukuu hizo mbili, Alisema hali aliyoikuta
Kituoni hapo inaridhisha kwakuwa abiria wote kwenye mabasi walikuwa wamepata
tiketi kwa bei elekezi ya Sumatra.
Dk. Mwakyembe alitoa wito
kwa abiria wote kuwa wahakikishe wanatoa ushirikiano kwenye vyombo vinavyohusika
pindi watakapotozwa nauli kinyume na ile ya kawaida.
“Msikubali kulipishwa zaidi
toeni taarifa haraka, hata katika nauli za mizigo msikubali kulipia mzigo wa
kilo 20 atakaekubali yote hayo mtambue amejitakia mwenyewe na asilaumiwe
mtu”alisema.
Naye Kaimu Mkurugezi
Udhibiti Usafiri wa Barabarani (Sumatra), Leo Ngowi, alisema katika operesheni
inayoendelea ya kuyakamata magari yanapandisha nauli holela jana, walifanikiwa
kulikamata basi la Kampuni ya KVC lenye usajili namba
T709AAT.
Alisema gari hilo
lilikwenda kinyume kwa kuwatoza nauli ya sh 35,000 baadala y ash 25,000 abiria
waliokuwa wakisafiri kwenda Arusha.
Aidha, Sumatra imetoa
leseni za muda kwa wamiliki magagri ambayo yamekidhi viwango vilivyohitajika na
mamlaka hiyo, yenye uwezo wa kuchukua abiria 30 kwa lengo la kusaidia
kusafirisha abiria wanaofika kwa wingi kituoni hapo ambapo mikoa inayoongoza kwa
abiria ni Kilimanjoro, Arusha na Mwanza.
Post a Comment