DAR ES
SALAAM-TANZANIA
Baada ya kuwasimamisha
viongozi saba, akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA),
Ephraim Mgawe, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, ameendelea na juhudi
za kutaka kuirejeshea hadhi mamlaka hivyo, na safari hii amewasimamisha kazi
viongozi wengine 16.
Dk Mwakyembe aliyasema
hayo jana alipozungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam,
akisema uamuzi wake umekuja baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo mengi
yanayokwamisha ufanisi wa shughuli za mamlaka hiyo.
Alisema Bodi mpya ya TPA
ilikutana na kupitia taarifa ya uchunguzi na baada ya kuipitia walichoamua ni
pamoja na kuwasimamisha viongozi wengine 16 na kufanya jumla ya viongozi
waliosimamishwa na kuandikiwa barua za kujieleza hadi sasa kufika
23.
Mwakyembe alisema hatua
ya kuwasimamisha wengine itaendelea itakapobainika nao wamefanya
makosa.
Alisisitiza kuwa, lengo
la hatua hiyo ni kuhakikisha hadhi ya bandari inarejeshwa na kuboreshwa zaidi
baada ya kubainika kuwepo kwa mapungufu mengi yaliyosababisha kupungua kwa
ufanisi wa shughuli za mamlaka hiyo.
Waliosimamishwa ni
Mkurugenzi wa Uhandisi, Mhandisi Mwandisi Bakari Kilo, Meneja Uhandisi, Mhandisi
Raymond Swai, Ofisa Mhandisi Mkuu, Mary Mhayaya, Mkurugenzi wa Mipango, Florence
Nkya, Meneja Ugavi na Ununuzi, Bahebe Machibya na Meneja Kitengo cha Ununuzi
(PMU), Theophil Kimaro.
Wengine ni Mkurugenzi wa
TEHAMA, Ayoub Kamti, Meneja Makasha, Mathew Anthony, Mkurugenzi wa Mifumo ya
Menejimenti,
Dk Maimuna Mrisha, Meneja TEHAMA, Marcelina Mhando, Ofisa Ulinzi, Fortunatus Sandaria, Kitengo cha Marine Fadhili Ngorongo, KOJ Opereta Owen Rwebangira, Diver Mohamed Abdullah na Opereta Kilimba.
Dk Maimuna Mrisha, Meneja TEHAMA, Marcelina Mhando, Ofisa Ulinzi, Fortunatus Sandaria, Kitengo cha Marine Fadhili Ngorongo, KOJ Opereta Owen Rwebangira, Diver Mohamed Abdullah na Opereta Kilimba.
Aliyataja baadhi ya
mapungufu yaliyobainika kwa mujibu wa taarifa hiyo ya uchunguzi kuwa ni kuwepo
mgongano wa kimaslahi ambapo viongozi wa ndani ya mamlaka hiyo wamekuwa na
kampuni zao ndogo ndogo zinazohudumia bandari.
“Huwezi kuendeleza
mamlaka ya bandari kwa mtindo huu. Kama una maslahi yako huwezi kusimamia
shughuli za mamlaka ipasavyo. Kama hiyo haitoshi tumekwenda hadi Brela hizo
kampuni hazijasajiliwa, ni za mfukoni tu,” alisema.
Alisema wote
waliobainika kuwa na kampuni hizo wameandikiwa barua wajieleze, kwa nini
wasichukuliwe hatua za kisheria. Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe ametoa
onyo kwa wale wote walioingia katika ajira kwa mipango bila sifa wajiondoe
wenyewe kabla hawajafukuzwa kazi.
Alisema moja ya kikwazo
cha ufanisi katika mamlaka hiyo ni ajira kutolewa bila kufuata taratibu na
Sheria za Nchi na kuonya kuwa wale wanaojijua wameajiriwa kwa mtindo huo waache
kazi wenyewe ili walipwe mafao yao badala ya kusubiri kuachishwa na kupoteza
kila kitu.
Waziri Mwakyembe pia
alizungumzia tatizo la kukithiri vitendo vya wizi ambavyo alivielezea kuwa na
mtandao mkubwa. Hata hivyo, alisema tatizo hilo litakomeshwa
kabisa.
“Haiwezekani kuruhusu
hali hii iendelee. Inakuwaje kontena nzima inayeyuka kama kiberiti, huu ni
mtandao mkubwa lazima tuukomeshe kabisa,“ alisema.
Alisema inatia aibu
kuona mapato ya Bandari ya Dar es Salaam kwa mwezi ni Sh milioni 27 hadi 28 kwa
mwezi wakati Mombasa ni Sh bilioni tatu. Hata hivyo alisema tangu mwezi Septemba
ufanisi mzuri umekuwepo hadi mapato yameongezeka.
“Wale walizoea mchezo
huu wa kuchuma kwa njia ya wizi nitawakamata, pamoja na wale wanaoiba vitu humu
ndani na kufanya biashara ya kuuza kwa kushirikiana na wale deiwaka wanaosimama
hovyo kwenye kijiwe nje, nitawakamata pia,” alisema.
Alipiga marufuku
utaratibu wa kulipisha mawakala Sh 200 kama pasi ya bandari (port pass) na
badala yake ametaka mamlaka
kuweka utaratibu wa kudhibiti watu kuingia hovyo na kuhakikisha kila mmoja ana kitambulisho kinachoeleweka na anajulikana
anakwenda wapi na anakwenda kufanya kitu gani.(CHANZO:HABARI LEO)
kuweka utaratibu wa kudhibiti watu kuingia hovyo na kuhakikisha kila mmoja ana kitambulisho kinachoeleweka na anajulikana
anakwenda wapi na anakwenda kufanya kitu gani.(CHANZO:HABARI LEO)
Post a Comment