Shirikisho
la mchezo wa soka nchini Uingereza FA, limewaandikisa barua makocha Harry
Redknapp na Roberto Mancini kuhusiana na shutuma zao dhidi ya
marefa.
Kocha
wa QPR, Redknapp, alimshutumu refa wa mechi yao siku ya Jumatano ambapo
walishindwa kwa magoli mawili kwa moja na West Brom.
Naye
kocha wa Manchester City Roberto Mancini, aliwashutumu maafisa walisimamia mechi
yao dhidi ya Sunderland, kwa kukosa kutoa adhabu baada ya nyota wake Pablo
Zabaleta kufanyiwa madhambi kabla ya Adam Johnson kufunga bao la ushindi la
Sunderland.
Makocha
hao wawili sasa wameamriwa kuwasilisha ripoti zao kuhusu matamshi waliyoyatoa
baada ya mechi zao.
Post a Comment