Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HABRI ZA KIMICHEZO ZA NYUMBANI ZILIZOTIKISA KWA MWAKA 2012

 

YANGA BINGWA KAGAME

Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame (Cecafe) Yanga wameweza kutetea vizuri ubingwa katika fainali ya kusisimua iliyochezwa uwanja wa Taifa, Temeke Dar es salaam
Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamisi baada ya kuibia pasi iliyorudishwa nyuma na beki wa Azam, ubunifu wa Rashid Gumbo, Haruna Niyonzima, katikati ulifanya kuweza kuliteka duara, na kuumpa wakati mgumu Salum Abubakar Sure Boy kuwa katika wakati mgumu, Dakika za majeruhi Said Bahanuzi aliweza kuzima ndoto za Azam baada ya kufunga goli la pili baada ya mabeki wa azam kwenda kushambulia hadi mpambano unamalizika Yanga 2-Azam 0

SIMBA BINGWA KOMBE LA URAFIKI

SIMBA SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.

Simba bingwa wa ngao ya Jamii
Azam imeshindwa kuchukua ngao ya Jamii ya TFF baada ya kushuhudia kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa Simba SC. Simba wakishinda kutokea nyuma baada ya kuwa tayari wameshafungwa bao 2-1 katika kipindi cha kwanza.
John Bocco aliipatia Azam bao la kuongoza katika dakika ya 5 na baadae Kipre Herman Tchetche akaongeza bao la 2 katika dakika ya 35.
Dakika ya 45 Daniel Akuffo aliipatia Simba bao la kwanza baada ya Mourad kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Mabao mawili kukamilisha ushindi wa 3-2 yalifungwa na Emanuel Okwi na Kazimoto.

YONDANI ASAINI YANGA


Kelvin Yondani akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mbele ya Seif Ahemd

MBUYU TWITE ATUA RASMI YANGA



Mbuyu Twite (kushoto) akiweka alama ya dole gumba katika mkataba wake mpya wa kuitumikia timu ya Young Africans wiki mbili zilizopita, kulia kwake ni mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Bin Kleb

NGASSA ATUA SIMBA

Azam FC Mabingwa wapya wa mapinduzi Cup, waifunga Jamhuri 3-1


Timu ya Azam FC imetwaa ubingwa wake wa kwanza mkubwa baada ya kulitwaa kombe la Mapinduzi 2012 kwakuwachabanga Jamhuri 3-1 katika mchezo wa fainali ya kombe hilo uliochezwa uwanja wa Amaan.
Azam FC wamefuta ndoto za Jamhuri za kutwaa kombe hilo na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni tano na medaliza dhahabu kwa kushusha kipigo hicho kilichiowaacha mashabiki wa timu hiyo kuondoka vichwa chini.
Safari ya Azam FC visiwani hapa imekuwa ya mafanikio kwa kupata kombe hilo linalofungua njia kwa makombemengine.

SIMBA SC BINGWA 2012

Mashabiki wa Simba SC kwa raha zao leo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top