MWANZA,
TANZANIA
WAKATI Chadema wamekuwa wakivuna kati ya sh.
milioni 36 na milioni 52 katika harambee zao mkoani Mwanza, kiasi hicho
kimeporomoka hadi kufikia sh. milioni 6 tu, katika harambee ya chama hicho
iliyofanyika Novemba 30, mwaka huu jijini humo.
Hali hiyo inatafsiriwa na wadadisi wa maswala
ya siasa hapa nchini kwamba, hiyo ni moja ya dalili za kuporomoka mvuto wa chama
hicho uliokuwa umeanza kutanda katika baadhi ya maeneo nchini.
Habari kutoka ndani ya chama hicho hapa jijini
Mwanza na kwa watu mbalimbali wakiwemo maarufu na baadhi ya
wafanyabiashara waliokuwa wamealikwa kwenye harambee hiyo ni kwamba wananchi
wamepunguza morari kwa Chadema kutokana na ubabaishaji wa viongozi wengi wa
chama hicho.
Katika harambee hiyo ya Mwanza, iliyofanyika
kwenye Hotel ya Gold Crest, ikiongozwa na John Mnyika ambaye ni Mbunge wa
Ubungo, kinyume na matarajio yake Chadema kiliambulia fedha taslimu sh.
6,180,000 tu.
Hiyo ni harambee ya tatu ya chama hicho
kufanyika hapa jijini Mwanza na pekee kuambulia fedha kidogo , ya
kwanza iliyofanyika katika hoteli hiyo kwa ajili ya kuchangia mfuko wa madawati,
zilipatikana zaidi ya sh. Milioni 38 kati yake Milioni 10 zikitolewa na rais
Jakaya Kikwete na ya pili iliyokuwa ya kuchangia madawati ambayo ilifanyika
mwanzoni mwa mwaka huu, kwenye uwanja wa Sahara zikapatikana sh. milioni
52.
Wakati Chadema wakiambulia kiasi hicho cha sh.
milioni sita, walikuwa wamekusudia kukusanya sh.Milioni 100 kutokana na
maandalizi ya harambee hiyo ambayo inasemekana yaligharim sh. milioni 15 hivyo
kuonekana kuwa ni hasara kulingana na kiasi cha fedha kilichopatikana.
“Hii yote ni kwa sababu ya ubabaishaji,
mkanganyiko, kauli na lugha za viongozi wetu akiwemo Mbunge wa jimbo
hili (Nyamagana) Ezekia Wenje.” Alisema mwanachama mmoja wa chama hicho, ambaye
alidai wakati wowote atatimka kwenye chama hicho.
“Mbunge wetu alikuwa akijiita mtoto wa mama
ntilie lakini sasa naye amekuwa mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya binaadamu,
labda harambee zetu ndizo wanafungulia maduka huko Dar es Salaam,
wanakon’gan’gania kuishi na kuwacha mama zao huku.”
Kwa mujibu wa viongozi wa M4C, wageni
walialikwa kwenye harambee hiyo walitoka katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni
Shinyanga, Simiyu, Mara, Kagera, Geita na Mwanza.
Viongozi hao walidai kuwa lengo la changizo
hilio ni kukiwezesha Chadema kupata fedha za kuendesha kampeni katika uchaguzi
mkuu ujao ili kiweze kushika dola mwaka 2015.
Post a Comment