Na Adnan Hussein, Mogadishu
Ndugu wa kikabila na washirika wa kiongozi wa
kikundi cha Kiislamu cha Hizbul Sheikh Hassan Dahir Aweys wamesema alikabiliwa
na hali ngumu huko Barawe, alizungukwa na waaminifu kutoka katika kabila lake
baada ya kunusurika majaribio kadhaa ya mauaji ya sababu za kisiasa.
Kiongozi wa
kikundi cha Kiislamu cha Hizbul Sheik Hassan Dahir Aweys (wa pili kutoka
kushoto) akitabasamu wakati wa sherehe za kusherehekea muungano wake na kikundi
kikubwa cha al-Shabaab tarehe 27, Disemba 2010. Vikundi hivyo viwili
viligawanyika tarehe 24 Septemba 2012, [Stringer/AFP]
Iman Nur, mwenye umri wa miaka 22 mwaminifu wa
Aweys, alisema kiongozi huyo amenusurika kama majaribio matano ya mauaji ya
sababu za kisiasa kwa wiki mbili zilizopita, jambo lililomfanya atafute ukimbizi
wa ghafla pamoja na kabila lake.
Nur alisema vitu vinavyotoka ndani ya
al-Shabaab vimekuwa vikijaribu kuzuia viongozi wenye msimamo wa wastani kama
Aweys kutojishughulisha katika mazungumzo na majadiliano ya amani pamoja na
serikali mpya.
Jaribio la hivi karibuni lilitokea tarehe 28
Novemba wakati wanamgambo wa al-Shabaab walipolenga gari la Aweys na chombo cha
mlipuko kinachodhibitiwa na rimoti katika barabara kuu ya Barawe, kilometa 170
kusini mwa Mogadishu.
Hakuna mmojawapo aliyekuwa kwenye gari
aliyejeruhiwa, lakini vipande vya bomu viliharibu gari lenye kuendeshwa kwa
magurudumu yote manne, kwa mujibu wa Mohamed Osman Aruus, aliyekuwa mpiganaji wa
al-Shabaab na ndugu wa Aweys.
Kikundi cha kiislamu cha Hizbul kiliachana na
al-Shabaab mwezi Septemba, kikinukuu tofauti za kiitikadi na mabadiliko ya
kisiasa nchini Somalia.
Mkaazi wa Barawe Sagal Khalif Abdi, mwenye umri
wa miaka 49, alisema mpaka uliowekwa kati ya waaminifu wa al-Shabaab na wale
walioondoka katika kikundi shirika cha al-Qaeda utaleta hali ya kutokuwa na
utulivu zaidi na umwagaji damu.
Alisema wapiganaji waliohusishwa na kiongozi wa
al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu al-Zubair,
waliweka vikwazo vikali katika njia za kuingilia kaskazini na kusini mwa
Barawe.
"Mmoja wa washauri wa Sheikh Hassan Dahir Aweys
walikwenda katika mji mkuu, Mogadishu, kuwahamasisha viongozi wa kikabila
kusuluhisha na kuanzisha mawasiliano kati ya Aweys na Rais wa Somalai Hassan
Sheikh Mohamud," Abdi alisema.
Hili lilifanyika baada ya mlolongo wa mabishano
na upinzani mkali kati ya waliokuwa washirika wa Aweys na Godane, alisema Abdi,
ambaye anatoka katika kabila hilohilo la Aweys.
Kuwadhoofisha al-Shabaab
Mchambuzi wa mambo ya siasa wa Somalia
Barkhadle Jibril Elmi alisema Aweys ameimarisha ulinzi wa kabila na amechukua
hatua za dhati kujilinda yeye na familia yake katika tukio la shambulizi
nyumbani kwake.
Elmi aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab
inajaribu kuwaondoa viongozi wa Hizbul Islam kwa sababu ya kuwa kwao tayari
kufanya mazungumzo na serikali na kukataa kufuata mawazo ya uharibifu ya kikundi
cha wapiganaji na vitendo vya magaidi.
Alisema jeshi la Somalia na vikosi vya misheni
ya Umoja wa Afrika huko Somalia wanapaswa kutumia nafasi ya hali ya kudhoofika
kwa kundi la wapiganaji na kuelekea Marka na Barawe ili kuwalinda watu na
kusaidia jitihada za amani na ungozi wa ndani.
Nasra Osman Jiiti, mwenye miaka 41, mwandishi
wa habari aliyestaafu, alisema mazungumzo ya Hizbul Islam na serikali ya Somalia
yatapunguza nguvu za al-Shabaab.
Alisema kikundi hicho kimekusudiwa kuanguka
kabisa kwa sababu kimewaua watu wasiokuwa na hatia na kufuja rasilimali zao.
Wanamgambo wa kikundi hicho wameelekeza bunduki zao dhidi ya mtu yeyote ambaye
anapinga mtindo wao wa kuwafyonza wapinzani, alisema.
"Hatujui nini kimetokea, lakini kila mmoja
anafikiria uwezekano wa kukabiliana kama tulivyoshuhudia mwezi Julai 2010 kati
ya al-Shabaab na Hizbul Islam kama walivyopigania rasilimali za kiuchumi kutoka
bandarini na uwanja wa ndege wa jiji la Kismayo, mji mkuu wa Lower Jubba,"
alisema.
Yasmin Salaad Gagale, mwanaharakati wa Chama
cha Kiraia cha Somalia, alisema ufunguzi wa mazungumzo ya kisiasa kati ya watu
wa kati dhidi ya al-Shabaab kutadhoofisha kikundi hicho na kutoa njia ya
operesheni za jeshi katika maeneo kadhaa ya Somalia ya Kati na ya Kusini.
Hili litasaidia kutekeleza mapendekezo ya
usalama yaliyokusudiwa katika kuwapiga al-Shabaab na wale wote wanaopinga amani,
alisema, akiongeza kwamba operesheni za jeshi zitaviwezesha vikosi vya kijeshi
vya Somalia kufuatilia wanamgambo na kuwazuia kutoroka na kuepuka adhabu kwa
uhalifu wao wa kuchukiza.
"Wahalifu wa ugaidi na washirika wao ambao
wamefanya mfululizo wa uhalifu dhidi ya wananchi wa Somalia wanapaswa
kukamatwa," Gagale aliiambia Sabahi. "Hawa ni watu ambao wameua, kukata vichwa
na kukata mikono, miguu na ndimi za watu bila ya sababu. Mamia ya watu watatoa
ushahidi kwa uhalifu wao, wakiwemo walionusurika katika mashambulizi ya mauaji
na uvamizi wao katika makazi ya jirani."
Gagale alisema mkakati kuhusu programu ya
usuluhishi ya taifa, ambayo lengo lake ni kuanzisha tena utulivu na udhibiti wa
serikali katika nchi nzima, ni kuwaruhusu wafuasi wa amani kuepuka na kutekwa na
wenye siasa kali.
Chanzo: sabahionline.com
Post a Comment